Mfalme wa kisingeli Tanzania, Msaga Sumu amefunguka kwa kumtaka Dulla
Makabila aache tabia ya kuweka tamaa mbele kwa madai anachokifanya
kinaweza kuwaaminisha watu kuwa waimba singeli wote ndivyo walivyo.
Msaga
Sumu amesema hayo baada ya Dulla Makabila kuwa na tabia ya kuchukua
'show' mbili kwenye usiku mmoja katika mikoa tofauti jambo ambalo...
ni
kinyume na taratibu za ujuzi wake anaoufanya kwa maana anakuwa
anawadanganya baadhi ya eneo.
"Nimeshaletewa mashtaka
mengi kwa mambo anayoyafanya mdogo wangu Dulla, siyo mara ya kwanza,
nimeshamuweka chini kuongea naye mara nyingi tu. Huwa namwambia kuwa
mkweli katika jambo moja, unapokuwa na tamaa utajiaribia halafu muziki
utakuja kuuwa kisha tutakuja kuonekana watu wote tunaoimba singeli ndiyo
tabia zetu zipo hivyo kumbe tofauti kabisa", amesema Msaga Sumu.
Pamoja na hayo, Msaga Msumu amesema siri
pekee ya kufanikiwa katika muziki ni kuwa na nidhamu jambo ambalo
linapelekea kupendwa na watu wa rika zote hata kama utakuwa hujui
kuimba.
"Ukiwa na nidhamu na heshima
katika muziki unaishi miaka mingi sana na kujuana na watu tofauti.
Utapendwa kwa sababu ya nidhamu pia nidhamu yako inaweza kukifikisha
mbali. Siku zote huwa namwambia mdogo wangu Dulla awe na nidhamu na ache
kauli za kavu kavu maana kuimba na kuongea ni tofauti", amesisitiza Msaga Sumu.
Katika hatua nyingine, Msaga Sumu
amesema ataendelea kubakia kuwa mfalme kwa madai katika nchi moja
hapawezi kuwa na wafalme wawili hata siku moja huku akiendelea kufafanua
kuwa wasanii wa sasa hawana ubunifu ndiyo maana sasa wamefeli katika
muziki wa singeli wanaofanya.
0 comments:
Post a Comment