Msanii wa bongo fleva asiyekaukiwa drama Zuwena Mohamed 'Shilole'
amedai kwa sasa ameshatolewa barua na mpenzi wake aliyeko naye kwenye
mahusiano na endapo Mungu akimjalia atafunga naye ndoa ili kuhalalisha, Shilole
amefunguka hayo na kusema kwa sasa ameamua
kuweka mahusiano yake faragha kidogo ili aweze kuwa huru na mpenzi wake.
"Mimi kwa sasa hivi sina
boyfriend kabisa, niwaambie tu nina mchumba ambaye tayari ameshanitolea
mpaka barua, Mungu akijaalia harusi...
nitawakaribisha siku siyo nyingi.
Na kuhusu wapenzi waliopita kuwa na mahusiano na marafiki zangu naona
ni kitu cha kawaida kwa sababu naamini mapenzi ni kama daladala ukishuka
mwenzako anakaa" alisema Shishi.
Kuhusiana na muziki wake msanii huyo
amedai anashindwa kutoa wimbo mpya kutoka na akaunti yake ya mtandao wa
instagram kudukuliwa na wahalifu wa mtandao.
"Nina miezi mitano tangu
nimeachia wimbo wa hatutoi remix najua masabiki zangu wamenimiss sana
lakini kinachonifanywa nishindwe ni kuwapa taarifa mashabiki zangu.
Dunia sasa ipo mikononi mwa watu na kwa wasanii inatusaidia kusukuma
kazi zetu " aliongeza
Kuhusu kolabo za kimataifa "Zipo nyimbo nyingi na nahitaji kuzitoa kwenye mpangilio mzuri siyo kutoa tuu nataka nitoe heavy song kila mmoja asubiri" alimaliza
0 comments:
Post a Comment