Pages

Subscribe:

Thursday, July 20, 2017

ANDER HERRERA AANZA KUPAISHA ROMELU LUKAKU

Herrera: "Ujio wa Lukaku umeongeza nguvu Man United"
Kiungo mahiri wa Manchester United amesema vita imeanza, na Mashetani Wekundu watakuwa tishio zaidi kufuatia ujio wa Romelu Lukaku, Ander Herrera amedai kuwa ujio wa Romelu Lukaku utawakosesha amani wapinzani wa Manchester United.

Mashetani Wekundu walishindwa kutakata Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita, hivyo kumlazimu Jose Mourinho kumleta nyota wa Everton kwa £75m. Mchezaji huyo tayari ana wasifu mzuri kwani amekuwa...
akifanya vizuri akiwa na West Brom na Everton ambapo msimu uliopita alifanikiwa kutikisa nyavu mara 25 na kuweka alama yake Ligi Kuu Uingereza.
 
Kufuatia kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic, Herrera amekiri kuwa United imepata nguvu mpya kwa ujio wa mchezaji huyo mahiri wa kimataifa wa Ubelgiji, mwenye umri wa miaka 24.
"Tuna wachezaji wengi kama Micki (Henrikh Mkhitaryan), Marcus [Rashford] na Anthony [Martial], ambao ni hatari sana mbele ya goli, lakini bado tulikuwa tunahitaji mtu kama Romelu," alikiambia MUTV.
"Ni shupavu na anaweza kukimbia na mpira. Wakati mwingine hata tukiwa tunakaba anaweza kutulia na mpira, kwa hiyo kazi anayofanya kwetu ni kubwa. Ni vigumu sana kumpokonya mpira, kwa hiyo atakuwa mtu muhimu kwetu."
United wameshinda mechi zao zote za maadalizi ya msimu, wakiifunga Los Angeles Galaxy 5-2 wikiendi na Real Salt Lake 2-1 Jumanne asubuhi.

0 comments:

Post a Comment