Pages

Subscribe:

Friday, July 28, 2017

SCRIPT YA NDANI YA JENEZA YAFUNGUA FURSA KWA G-NAKO



Msanii wa Bongo Flava, G Nako mara baada ya kuachia video ya ngoma yake yake ‘Lucky Me’ ambayo anaonekana akiwa amelala kwenye jeneza, ameeleza kuna baadhi ya madirector wa video wamemfuata na kutaka kufanya nae kazi.

Rapper huyo kutoka kundi la Weusi amedai kuwa madirector hao walimpongeza kwa alichokifanya huku wakisema waigizaji wengi wamekuwa wakishindwa kufanya kama yeye kutokana na...
uoga.

“Wamenifuata, kuna madirector wameniambia kazi uliyofanya pale ni nzito, kwa hiyo labda tunaweza tukaa chini tukazungumza kufanya kazi nyingine,” amesema G Nako na kuongeza.

“Nikipata mtu ambaye ana concept nzuri, ana vitu vya tofauti na hivi ambavyo tumezoea kuona kila siku nafikiri nitaingia kwenye hiyo sekta. Kuna baadhi ya vitu tushavifanya vipo chini ya carpet lakini kwa sasa siruhusiwi kuvisema  ila napenda kuigiza,” amesisitiza.

Video ya Luck Me ya G Nako ilitoka June 17 mwaka huu ikiwa imeongozwa na Hanscana na hadi sasa imetazamwa mara 168, 388 katika mtandao YouTube.

0 comments:

Post a Comment