Mwanamuziki anayefanya vizuri na ngoma yake ya 'Nibebe', Beka Flavour
amefunguka na kusema Aslay siyo msanii mkubwa wa kumuangalia wakati
anafanya kazi zake na badala yake Alikiba ndiye kioo chake kwa Tanzania.
Beka
amelazimika kusema hayo baada ya kuwepo minong'ono kuwa huenda
anamuogopa msanii huyo ambaye zamani walikuwa wakifanya kazi pamoja kama
kundi la 'Yamoto Band' kabla ya kila msanii kuanza...
kusimama mwenyewe.
"Mimi natoa nyimbo zangu
kulingana na jinsi ambavyo nimepanga ratiba yangu na uongozi wangu.
Sijashindwa kuachia wimbo eti kwa sababu Aslay katoa ngoma mpya ila
matatizo niliyopata ya kupelekwa polisi ndiyo yaliyonifanya nisogeze
vitu mbele," Beka alifunguka mbele ya kamera za eNewz
Beka aliongeza kuwa "Aslay
siyo msanii mkubwa kusema kwamba mimi nimuogope au nimfikirie. Hapa
nchini msanii mkubwa ni Alikiba na ndo kama kioo najitazama lakini siyo
Aslay. Mimi natazama wasanii wakubwa nje ya nchi lakini siyo ndugu
yangu".
Pamoja na hayo Beka amedai hataweza
kumvumilia tena msanii huyo ambaye amefululiza kutoa nyimbo nyingi hivi
karibuni endapo ataachia tena kazi mpya.
"Nimepanga kuachia wimbo
mpya wiki mbili zijazo lakini kama Aslay akiachia tena kazi mpya
sitaweza kumvumilia na mimi nitaachia mashine ili zipambane mbele kwa
mbele maana mimi nimeshapanga ratiba zangu na siwezi kuzivunja," aliongeza.
0 comments:
Post a Comment