Msanii Baraka The Prince amefunguka kwa kudai sababu kubwa zilizomfanya
yeye kujiengua katika usimamizi wa kampuni ya RockStar4000 ni kutokuwa
makini na ukweli katika kazi wanazozifanya dhidi yake.
Baraka
amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuona
takwimu zake zimezidi kushuka katika kazi zake alizokuwa anasimamiwa na
uongozi huu pamoja na kutolewa... nyimbo moja kwa mwaka tofauti na yeye
alivyokuwa anategemea atafanya.
"Nimeamua kufanya hivyo kwa
sababu hii ndiyo kazi yangu na mwisho wa siku hii mimi ndiyo kila kitu
na sina kazi nyingine, kwa hiyo nikiona kuna vitu havipo 'serious' na
havipo 'sure' kwa upande wa watu ninaofanya nao kazi sina budi kujiengua
na kufanya mwenyewe. Nipo sawa na hakuna mtu ambaye anaweza kuniingilia
juu ya hilo mwisho wa siku mimi ndiyo ninajua kazi ninayofanya na ugumu
wake katika kujenga 'brand' yangu, najua ugumu wa kila kitu 'so' haya
ni maamuzi yangu", amesema Baraka.
Pamoja na hayo, Baraka ameendelea kwa kusema "mimi
ndiyo mwenye kauli ya mwisho. Sitaki kuongelea masuala ya mikataba kwa
sababu kipindi nina saini tokea awali sikuweza izungumzia wakati naingia
kwa hiyo sitasema lolote juu ya hilo kwa sasa",amesisitiza Baraka.
Kwa upande mwingine, Baraka amesema yeye
hafanyi muziki kwa ajili ya menejementi bali anafanya muziki kwa
mashabiki wanamuwezesha kumlipa katika nyimbo zake wanazozipakua katika
mitandao.
0 comments:
Post a Comment