Msanii wa bongo fleva na mpenzi wake Baraka the Price, Najdattani
amefunguka kwa kukanusha kuwa hajawahi pigwa marufuku na mwenzake wake
kuwatumia 'model' wa kiume katika video yake mpya ya wimbo wa utanielewa
kama watu wengine wanavyodai.
Naj
amebainisha hayo baada ya kuwepo
minong'ono mingi inayodai kuhusisha wivu wa kimapenzi katika kazi mpaka
kupelekea mwanadada huyo kukataa...
kuwaweka wanaume katika video yake kwa
kuwa watamshika shika mwili wake.
"Hanibani kwenye kazi zangu
kiukweli na hata hajawahi kuniambia oonh sitaki uweke ma-model sijui
nini na nini hata hatujawahi kufikilia mazungumzo hayo lakini
nilivyomwambia kuhusiana na 'idea' hata mwenyewe pia alichangia kwenye
hilo akasema hiyo ni nzuri itakuwa kitu cha utofauti kabisa hatujawahi
kuwa na tatizo", amesema Naj.
Pamoja na hayo, Naj amesema siyo lazima mwanaume aonekane katika video ya wimbo wake japokuwa maudhui ya wimbo hiyo ni mapenzi.
"Ujumbe ukiuangalia vizuri
utaona ni mwanamke ambaye anampenda mwanaume fulani hivi lakini yeye
hajamkubali kwa kipindi hicho na endapo pale unapoamua ku-move on, yeye
ndiyo anaanza kuja yaani mnapishana 'so' ndiyo maana siyo lazima hata
mtu mwenyewe aonekane", amesisitiza Naj.
Kwa upande mwingine, Naj amewataka watu
na mashabiki zake waziondoe hizo fikra katika vichwa vyao ya kwamba wivu
wa mpenzi wake ndiyo umesababisha kutoonekana video model wa kiume
katika wimbo wake.
0 comments:
Post a Comment