Mkali wa muziki wa singeli Bongo, Man Fongo amekubali yaishe baada ya
kumaliza tofauti zilizokuwepo kati yake na meneja wake wa zamani, kutoka
'Makers Entertainment' G Maker kwa kurudi na kuomba radhi.
Msanii
huyo aliyetamba na ngoma ya ‘Hainaga ushemeji’ mwaka 2015 akiwa chini
ya usimamizi wa G Maker, aliingia katika ‘bifu’ kali na meneja wake huyo
katikati ya mwaka 2016- 2017 huku chanzo kikitajwa kuwa ni...
kutofautiana
katika suala la pesa.
Baada ya kutengana kwa takriban mwaka
mmoja, Man Fongo ambaye ametambulisha rasmi ngoma yake mpya jana
aliyoipa jina ‘popcorn’, amesema aligundua kosa lake na kuamua kurudi
kwa G Maker, kwa kuwa aliona hawezi kuwa mbali naye kikazi kutokana na
uhusiano wao kama ndugu.
Ngoma ya Man Fongo aliyoiachia jana ipo
chini ya uongozi wa G Maker na huku mpikaji wa ngoma akiwa ni Mensen
Selekta ambaye kwa pamoja hiyo ndiyo timu iliyotengeza 'hit' ya 'Hainaga
Ushemeji'.
Msanii huyo amesema video ya ngoma hiyo ipo katika hatua za mwisho, na wakati wowote itakuwa hewani.
0 comments:
Post a Comment