Pages

Subscribe:

Friday, July 21, 2017

PAM D: MIMI KUREKODI KWENYE STUDIO YA NAY SIYO DHAMBI

Baada ya uvumi mtaani kuhusu kugombana kwa wasanii ambao ni ndugu, Pam D pamoja na Mesen Selekta, wawili hao wamekanusha kuwa na ugomvi na kuongeza kwamba kazi haziwezi kuwatenganisha kwani wao ni familia moja. 

Mesen pamoja na Pam D wameweka wazi baada ya kubananishwa na kamera za eNewz kutokana na kutokuonekana kwao karibu huku kila mmoja akishindwa kuonyesha ushirikiano katika...
kazi za mwenzake.

"Mimi siwezi kugombana na Mesen kwa sababu yule ni kaka yangu, na hata ninapokuwa nakosea huwa ananielewesha na tunashauriana mambo mengi. kuhusu kunisapoti saizi yeye ana kazi yake ambayo anatakiwa ai-push sidhani kama ni muda sahihi wa kuhangaika na mimi', amesema Pam D 

Kuhusu kuhama kufanya kazi kwenye studio ya Mesen, Pam D amesema kwamba "Mimi kwenda kurekodi kwenye studio ya Nay wa Mitego siyo dhambi kwani yule ni rafiki yangu na Mesen alikwishanipa baraka zote na uzuri ni kwamba ananielewa mimi mdogo wake ni mpambanaji kwa hiyo hakuna kinachoharibika", aliongeza.

Kwa upande wake Mesen amedai haelewi maneno yanatoka wapi na kuongeza kwamba yeye na Pam D katu hawawezi kugombana ingawa pia katika mkataba wake mpya aliosaini hivi karibuni hakuweza kumshirikisha kwani suala la pesa lingeweza kuharibu mahusiano yao.  

0 comments:

Post a Comment