Msanii kutoka kampuni ya Weusi Niki wa Pili amewapa ushauri vijana
waliozaliwa katika ardhi ya Tanzania kwa kuwaambia waache kufuta mifumo
au mitazamo isiyo akisi katika ujana wao na badala yake wajitume katika
kupambana na hali ya maisha ili waweze kufanikiwa maisha kabla ya miaka 38.
Nikki amesema hayo kupitia ukurasa wake
wa Instagram baada ya kuwepo kundi kubwa la vijana mtaani huku wengine
wakiamini kwamba hawawezi kufanikiwa maishani mwao mpaka wawe na...
mtu
pembeni yao wa kumpa msaada wa kumshika mkono ili aweze kufika mahali
fulani.
"Tanzania kuna utamaduni
mkubwa wa kuwapangia vijana cha kufanya, kusema hata kuvaa. Huko
mashuleni au vyuoni sauti za vijana, wanafunzi hazina nafasi katika
kuandaa mitaala wala namna ya kuendesha vyuo au shule kila kitu
kinapangwa na walio wakubwa zaidi ndiyo maana kufanikiwa wengi wanaanza
juu ya miaka 38", ameandika Nikki wa Pili.
Pamoja na hayo, Nikki ameendelea kwa kusema "Vijana
msifuate mifumo au mitazamo isiyo akisi ujana wenu, nguvu yenu na ndoto
zenu. Msisubiri vitoke juu kwa wakubwa kama msaada, anzieni chini
mjifunze kupitia nyie kwa nyie", amesisitiza Nikki.
Kwa upande mwingine, Nikki amesema hata
katika madarasa ya elimu ya juu (masters) hakuna uhusishwaji wa sauti za
wanafunzi katika kufanya jambo lolote lile ila kinachoangaliwa ni jinsi
gani umelipa karo ya masomo na kuingia darasani na kufundishwa tu.
0 comments:
Post a Comment