#1Eric Cantona - 1992 - paundi milioni 1.2 kutoka Leeds United
Msimu
wa 1992 Manchester United waliuanza kwa kufanya sajili mbili, Dion
Dublin kutoka Cambridge United na Erick Cantona kutoka Leeds. Dublin
alikuwa chaguo la pili kwa Ferguson baada ya kushindwa...
kumnasa Alan Shearer ambaye alijiunga na Blackburn Rovers.
Dublin aliishia kufunga goli mbili kwenye Ligi kuu kabla ajaondoka Old Trafford 1994 lakini kwa upande wa Cantona mambo yalikuwa tofauti kwani alikuja kufanya mambo makubwa Old Trafford. Katika miaka 5 ya alifanikiwa kushinda mataji mann4 ya Ligi Kuu, manne ya kombe la Carling na mawili ya FA.
kumnasa Alan Shearer ambaye alijiunga na Blackburn Rovers.

Dublin aliishia kufunga goli mbili kwenye Ligi kuu kabla ajaondoka Old Trafford 1994 lakini kwa upande wa Cantona mambo yalikuwa tofauti kwani alikuja kufanya mambo makubwa Old Trafford. Katika miaka 5 ya alifanikiwa kushinda mataji mann4 ya Ligi Kuu, manne ya kombe la Carling na mawili ya FA.
#2Roy Keane - 1993 - paundi milioni 3.75 kutoka Nottingham Forest

Roy
Keane alikuwa ndiye mchezaji ghali Uingereza pindi alipokuwa ana hamia
United katika kipindi chake . Ndani ya muda mfupi kiungo huyo alikuja
kuwa moyo wa timu, alifanikiwa kucheza mechi 480 na kushinda mataji 7 ya
Ligi Kuupamoja na Ligi ya Mabingwa mwaka 1999mechi ambayo kiungo huyo
hakucheza kutokana na kutumikia adhabu ya kadi.
#3Andy Cole - 1995 - paundi milioni 7 kutoka Newcastle
Ndani ya muda mfupi Andy Cole alifanikiwa ndani ya Manchester United na kuwa mtambo muhimu wa magoli pale Old Trafford, ameisaidia klabu kushinda mataji mbali mbali katika kipindi chake kama Ligi Kuu, Ligi ya mabingwa, FA na mataji mengine.
#4Ole Gunnar Solskjaer - 1996 - paundi milioni 1.5 kutoka Molde
Ni
nyota wa kukumbukwa sana pale Manchester United, Mnorway huyo alikuwa
supa sabu bora duniani katika kipindi chake, alisajiliwa na Ferguson
baada ya wapinzani wao klabu ya Man City kugoma kumsajili,
anakumbukwa zaidi mwaka 1999 kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa pale
alipotokea benchi na kwenda kufunga goli la ushindi dhidi ya Bayern
Munch.
#5Teddy Sheringham - 1997 - paundi milion 3.5 kutoka Spurs
Teddy
aliletwa kwa ajili ya kuja kuziba pengo la Erick Cantona ambaye
alistafu kwa kipindi kifupi tu , amecheza kwa mafanikio makubwa katika
muda wake na kushinda mataji mengi, ana kumbukwa na mashabiki wengi wa
United mwaka 1999kwenye fainali ya ligi ya mabingwa pale anatokea benchi
na kwenda kusawazisha goli dhidi ya Bayern Munich.
#6Jaap Stam - 1998 - paundi milioni 10 kutoka PSV
Mwaka
1998 United walivunja rekodi yao ya usajili mara mbili kutokana na
usajili wa Jaap Stam na Dwight Yorke, Stam alikuja kuwa beki bora
Duniani katika kipindi alichoitumikia Man United na kushinda mataji yote
Old Trafford.
#7Ruud van Nistelrooy - 2001 - paundi milioni 19 kutoka PSV

Ruud
van Nistelrooy ni moja wa wafungaji bora wa United, amefanikiwa kufunga
magoli 150 katika mechi 219, pia alifanikiwa kuvunja rekodi mbali mbali
akiwa Old Trafford.
#8Rio Ferdinand - 2002 - paundi 29.1 kutoka Leeds United

#9Cristiano Ronaldo - 2003 - paundi milioni 12.24 kutoka Sporting CP
Ni
mmoja wa wachezaji bora wa muda wote Manchester United, amefanya mambo
makubwa ndani ya United kabla ajauzwa kwenda Real Madrid kwa uhamisho
uliovunja rekodi paundi milioni 80, ndani ya Old Trafford amefanikiwa
kushinda mataji kadhaa yakiwemo ya Ligi Kuu, FA, na Ligi ya mabingwa.
#10Wayne Rooney - 2004 - paundi milioni 27 kutoka Everton

#11Edwin van der Sar - 2005 - paundi milioni 2 kutoka Fulham

Baada
ya kuhusishwa kwa muda mrefu na kujiunga na Manchester United hatimae
mwaka 2005 Van der Sar alijiunga na United akitokea Fulham na kuja
kuziba pengo kubwa la golikipa ambalo lilikuwa ni changamoto pale Old
Trafford katika kipindi hicho, ndani ya kipindi kifupi alifanya kazi
kubwa na kuiwezesha klabu kushinda mataji mbali mbali.
#12Nemanja Vidic - 2005 - paundi 7 kutoka Spartak Moscow

Alikuja
kutengeneza safu bora ya ulinzi yeye pamoja na Rio Ferdinand na
kuifanya kuwa ngome ngumu kupitika katika Ligi Kuu ya Uingereza,
alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu mwaka 2009 baada ya kuiwezesha
timu kutoruhusu goli katika mechi 14 mfululizo.
#13Michael Carrick - 2006 - paundi milioni 14 kutoka Spurs

#14Dimitar Berbatov - 2008 - paundi milioni 30.75 kutoka Spurs
Berbatov
alikuwa na nafasi kubwa ya kujiunga na Manchester United kabla ya
Ferguson kwenda kumuiba katika dakiaka za mwisho, amefunga magoli mengi
pale United na kuja kuwa kipenzi hasa baada ya kufanikiwa kuwafunga
Liverpool magoli matatu pekee yake.
#15Antonio Valencia - 2009 - paundi milioni 16 kutoka Wigan

Tangu
enzi za Sir Alex Ferguson hadi sasa kwa Mourinho, Valencia amekuwa
mchezaji muhimu, amekuwa akitumika kwenye maeneo tofauti tofauti
uwanjani na kutimiza majukumu kwa asilimia kubwa.
#16Javier Hernandez - 2010 - paundi milioni 7 kutoka Guadalajara

Alijiunga na United mwaka 2010 baada ya kombe la Dunia lililofanyika Afrika Kusini, Chicharito alikuwa akifananishwa na Ole Gunnar Solskjae kutokana na staili yao wanayocheza, nyota huyo alikuwa na uwiano mzuri wa kufunga licha ya kuwa anatokea benchi
#17David de Gea - 2011 - paundi milioni 18.9 kutoka Atletico Madrid

#18Robin van Persie - 2012 - paundi 22.5 kutoka Arsenal

Kitendo
cha Van Persie kujiunga na United kiliwaumiza sana mashabiki wa Arsenal
na kuchukulia kama usaliti, ndani ya msimu wake wa kwanza Mholanzi huyo
alifanikiwa kuwa mfungaji bora na kunytakuwa taji la Ligi ya Kuu Old
Traffor.
#19Paul Pogba - 2016 - paundi milioni 89 kutoka Juventus

Usajili
uliovunja rekodi ya klabu na Dunia kipindi anajiunga na United akitokea
Juve, Pogba alikuwa na presha kubwa nyuma yake kutokana na pesa zilizo
tumika kwenye usajili wake lakini taratibu presha inapungua na mchezaji
huyo ameanza kuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha United




Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment