Kwa
mara ya kwanza katika soka la Afrika Teknolojia ya msaada wa video kwa
waamuzi wa soka, maarufu kama VAR (Goal Technology), utaanza kutumika
kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika CHAN kwa wachezaji
wanaocheza ligi za ndani yatakayofanyika Morocco.
Mfumo huo unaruhusu maafisa walioko
nje ya uwanja kusaidia waamuzi walioko ndani ya uwanja katika masuala
kama goli linapoingia, penalti, kadi nyekundu na inapotokea mchezaji...
ameadhibiwa kwa makosa. Mfumo huo umetumika katika ligi ya Italia Serie A na Bundesliga nchini Ujerumani.
Teknolojia hiyo inatarajiwa kuanza kutumika nchini Morocco wakati michezo hiyo itakapofikia robo fainali , ambapo timu zinazoshiriki zinatumia wachezaji wanaocheza ligi za ndani. Timu 16 zinashiriki.

Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment