Pages

Subscribe:

Tuesday, January 2, 2018

JAY MOE: NCHI NYINGINE HAKUNA UTARATIBU WA LABEL LAKINI HIP HOP INAFANYA VIZURI



Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Jay Moe ametaja sababu ya muziki huo kushindwa kufanya vizuri zaidi kimataifa. Rapper huyo ambaye anatamba na ngoma ‘Bata’ ameiambia XXL ya Clouds Fm sababu ya wasanii wengi kushindwa kufanya hivyo ni kutokana na kufanya kazi nje ya label.

“Wengi wanafanya muziki wao nje ya label, kwa hiyo leo ukitaka kumfananisha Fid Q ambaye hayupo kwenye label yoyote zaidi ya Cheusi Dawa ambayo anaimiliki mwenyewe leo tukamfananishe na...
Mr. Incredible ambaye yupo chini ya Chocolate City au Fino, Cassper Nyovest  hao wameshajitangaza,” amesema Jay Moe.

Jay ameongeza kuwa kuna nchi nyingine hakuna utaratibu wa label lakini kuna kampuni kubwa ambazo zinawekeza katika muziki huo kitu kinachofanya kuendelea kukua.

“Au hata Kenya hiyo ilikuwepo, unakuta hamna label lakini huyo msanii ana mkataba na MTN kwa hiyo kuna pesa nyingine zinapatikana kule,” amesisitiza.
Pia ameongeza wasanii hip hop wenyewe wameshindwa kutengeneza maudhui ya kibishara ambayo yanaendana na soko la sasa.

0 comments:

Post a Comment