Pages

Subscribe:

Tuesday, January 16, 2018

MBUNGE SUGU APELEKWA GEREZANI BAADA YA KUKOSA DHAMANA

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi leo Januari 16, 2018 amepelekwa mahabusu katika gereza la Rwanda jijini Mbeya baada ya kukosa dhamana kufuatia kesi inayomkabli ya kutoa maneno ya uchochezi katika moja ya mkutano wake .

RPC wa Mbeya akiongea amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Mbunge huyo leo alipelekwa mahakamani kwa kosa hilo na mahakama imemnyima dhamana na ...
kupelekwa katika gereza la Rwanda. 

"Leo tulimpeleka mahakamani kutokana na Mkutano wake wa hadhara ambao aliufanya tarehe 31 Disemba mwaka jana kuna maneno ambayo alitamka hayakuwa mazuri kwenye ule mkutano pamoja na kwamba katika maombi yake kwenye huo mkutano alisema anataka anataka kuzungumzia maendeleo pamoja na kuwatakia kheri ya mwaka mpya 2018 lakini matokeo yake alizungumza mambo mengine ambayo yanaweza kujenga chuki kati ya wananchi na serikali kwa hiyo tulipeleka jarada kwa wanasheria wa Serikali ikaonekana kuna makosa ya kujibu mahakamani kwa mujibu wa sheria" 

Aidha RPC huyo aliendelea kusema kuwa baada ya kupelekwa mahakamani Mbunge huyo amenyimwa dhamana na kupelekwa magereza. 

Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Jongwe’’ pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga imetajwa leo Jumanne tarehe 16 Januari, 2018 katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya na mahakama imewanyima dhamana na kuamuru wapelekwe rumande mpaka tarehe 19 Januari 2018.

0 comments:

Post a Comment