Msanii wa mziki na filamu Gelly wa Rhymes amejibu fununu zisemazo yeye ni chawa wa Hemed na hana mchongo mwengine wa maana mjini kwa kusema yeye na Hemed ni zaidi ya ndugu.
Akipiga
story kupitia eNEWZ ya East Africa Television Gelly amesema yeye na
Hemed wamepita hatua za urafiki na sasa wapo kama ndugu kwa kuwa
wamepitia mambo mengi sana na wamekuwa...
wakisaidiana mambo mengi sana kiasi kwamba kwa sasa wanaishi kama mtu na kaka ake.
''Watu wanaosema mimi ni Chawa wa Hemed basi wafahamu kwamba hata Hemed ni chawa wangu kwasababu sisi tunashirikiana kwa mambo mengi'', amefunguka Gerry. Gelly pia amefunguka kuwa yeye na Hemed Phd wana mpango wa kuanzisha 'Lebel' yao ambayo itakuwa na wasanii na pia itasimamia mziki wao.
Gelly amemalizia kwa kusema kwamba nyimbo yake mpya inayokuja anampango wa kuwachana 'Vibenten' wote ambao wanaishi mjini kwa kuwategemea wanawake wawaletee hela ambazo wanahongwa na wanaume wengine. Amesema wengine ni watu maarufu na atawaja kwa majina.

0 comments:
Post a Comment