Pages

Subscribe:

Friday, January 12, 2018

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya 15) - 15

Related image
Sehemu ya:15 

Maneno yale yakufanya Mark ajisikie vibaya aliaga pale sebuleni nakuondoka, Baraka akasema "tunashukuru sana, ila naomba utuonyeshe chumba chakulala", Suzy akasema "itabidi mlale hapa sebuleni maana siwezi walaza chumbani na mtoto mdogo asije kojoa mkaharibu godoro tena, usiku mwema jamani kisha aliondoka kuelekea chumbani.

Mama Prisca alianza kulia"Suzy ananifanyia mimi hivyo, anasahau mimi ndiye niliyemleta mjini tena bahati yake mwanangu anaumwa ningempiga leo", Baraka alitikisa kichwa kwa kusikitika kisha alianza...
kucheka, alicheka sana kisha akasema"mke wangu umeona mke uliyemletea kaka yako, katunyima chakula, anatulaza sebuleni hajali ata hali ya mgonjwa, unadhani kaka yako anaishi vipi?, 

kama sisi wageni hivi", Mama Prisca alisema sikujua Baraka na wazazi walimpenda kwani alikua na nidhamu sijui kakumbwa na nin?, yaani yeye anatufanyia hivi bila shaka mdogo angu anateseka sana sijui nitafanyaje maana anaonekana mjamzito, 

Baraka akasema sio anaonekana ni mjamzito Yule, mama Prisca akasema"au hali hiyo ndiyo inasababisha maana watu wakiwa na mimba wanasumbua, Baraka aliposikia hivyo alicheka tena huku akisema "basi kumbe mimba hiyo kiboko maana haina adabu hata kidogo", waliongea kwa muda bila kulala mpaka usingizi uliwachukua. 

Walilala mpaka asubuhi Mark alipoamka alishangaa kuwaona ndugu zake sebuleni na alipouliza Baraka alijibu"jana Prisca katusumbua sana tukajikuta tumelala hapa", hakutaka tena habari za Suzy ndiyo maana hakusema lolote. Basi Mark aliwaambia wajiandae waende hospitali, basi wote walianza kujiandaa walipomaliza wakaondoka na kumuacha Suzy nyumbani,. 

Walifika hospitali walimpa daktari ile barua, daktari aliahangazwa na taarifa ile kuhusu ile barua na baadae aliwachukua damu na kuwaomba wasubiri majibu, daktari baada ya kurudi alirudi akiwa na hali ya hudhuni sana, aliwaita na kuwapa majibu kama yale yale ya mwanzo, watu wote walishangaa na Mark aliuliza hali hii inawezekana vipi?daktari alijibu "tangu nianze kazi ndiyo mara yangu ya kwanza nakutana na hali hii sijawahi kutana nayo, hapa cha muhimu binti huyu aanze dawa mapema ili kuongeza siku zake zakuishi", daktari aliamaliza. Mama Prisca alilia sana.., usikose 16

0 comments:

Post a Comment