Tuesday, January 16, 2018
STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya 17) - 17
Sehemu ya:17
Usijali alishawasamehe zamani wala hana kinyongo na yeyote na nilipomuambia umejifungua alitamani kuja kukuona lakini aliogopa, hanaga shida Yule, basi walipomaliza Mark alianza kuwasindikiza wageni zake nje ili wakapande gari waondoke.
Kipindi hayo yote yanaongelewa Suzy aliyasikia yote kwani alikua kasimama mlangoni akisikiliza, walipotoka nje akasema"kumbe ile dawa haijakolea kabisa, bado anawasiliana na...
Yule mwanamke kumbe, kumuachia kidogo tu shida, ananiletea utani mimi kumbe hajanijua vizuri huyu mwanaume, na huyo Baraka hana hata undugu wa damu anajitia ushauri, ndiyo maana anapatwa na matatizo kisa kidomo sijui ata kitoto chao kinaumwa nini si kife tu.
Yaani Suzy haamini kama ni mimi hahahhahahah mambo ya mjini na bado maana nina mpango wakumvuruga huyo mwanaume mpaka nibaki na mali zote hizi kwanza nachelewa", akachukua simu na kupiga alisema, "rafiki yangu mwenzangu hili jitu langu dawa haijamkolea fanya mipango unirudishe kwa babu sawa, alisikika akicheka kisha akakata simu na kutabasamu.
Basi Mark baada ya kuwasindikiza ndugu zake alirudi nyumbani na akabadilisha nguo kisha aliondoka. Suzy alijisemesha "kaage baba maana nikienda kwa babu hutorudi tena huko", basi Mark alifika kwa mama Careen alipokelewa kwa furaha na mwanae wa kufikia Careen, walicheka na mama Careen kisha akamuhadithia yaliyomkuta dada yake.
Mama Careen alisikitika sana akasema"angekua mkubwa angeishi nae uenda angeombewa anaposali labda angepona", Mark akasema "siunajua bado mdogo anahitaji sana malezi ya wazazi wake kisha akasema"mke wangu naomba unisamehe sana kwani halikua lengo langu mimi kuishi na Yule mwanamke, mama Careen akasema"najua mume wangu ndiyo maana nipo na wewe mpaka leo, mark aliendelea"nakuamini sana mke wangu leo nimeleta baadhi ya vitu vyangu muhimu nikiwa na vihitaji ntavifuata kwako ni hati ya nyumba na vitu vingine muhimu pia nyumba hii inatikiwa ukaishi wewe mimi nikiweka mambo sawa nitakuja sio vizuri kuendelea kulipia hapa na nyumba ipo, mama Careen alifurahi sana lakini akasema"kwanini ninyi msiende ishi kule maana pale unapoishi rafiki yako akirudi itakuaje?,
usikose 18
Labels:
HABARI & UDAKU,
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment