Pages

Subscribe:

Saturday, April 11, 2015

DIAMOND KUJA NA COLABO YA KUTISHA KUTOKA AMERICA


Diamond Platnumz is unstoppable! Ni muda mrefu sasa tumekuwa tukisikia tetesi kuwa amerekodi ngoma na msanii mkubwa wa Marekani japo hakuwahi kumtaja, Muimbaji huyo alikuwa akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV leo asubuhi ambapo aliulizwa ni msanii gani wa nje ya Afrika anayependa kufanya naye kazi.

Diamond alidai kuwa tayari msanii anayemkubali zaidi nchini Marekani ameshafanya naye kazi japo...

hakupenda kumtaja tena.

Aliombwa amtaje msanii mwingine tofauti na huyo na kusema wasanii watano anaowapenda zaidi nchini Marekani ni Nicki Minaj, Chris Brown na Usher Raymond na kwamba mmoja kati ya hao tayari ameshafanya naye ngoma!

Kwamujibu wa mtandao wa Bongo 5 wao wame bashiri kuwa kwakuwa inafahamika Diamond Platnumz anamkubali Usher Raymond basi inawezekana atakuwa ndiye msanii waliye fanya naye kazi hiyo.

0 comments:

Post a Comment