skip to main |
skip to sidebar
DIAMOND ATOA SABABU YA KUSITISHA KUACHIA WIMBO MPYA
Diamond Platnumz
MWANAMUZIKI wa Afro Pop, Diamond Platinum anatamani kuachia ngoma nyingine
lakini amekiri kupata kikwazo kutokana na matokeo ya Wimbo wa Nana
aliouachia mara ya mwisho.
Diamond au Chibu amefunguka kuwa kwenye ‘library’ yake ana nyimbo nyingi
kali ambazo zipo tayari kuachiwa muda wowote lakini kutokana na...
Nana
kuendelea kufanya vizuri mpaka sasa tangu alipoiachia anaona bora aendelee
kusubiri, asifululize kuingiza kazi nyingi sokoni kwa wakati mmoja.
“Unajua vitu vipya vipo, lakini nimecheki upepo naona kama bado kwanza kwa
sasa maana Nana bado inafanya vizuri,
nataka
kuipa muda kwanza kabla sijaachia ngoma mpya japokuwa nia yangu kubwa ni
kuachia wimbo kabla ya mwaka haujabadilika, kwa hiyo bado nacheki,” alisema Diamond.
Nana ambao amemshirikisha Flavour wa Nigeria, umewika vizuri Afrika na
kufanikiwa kumpa baadhi ya tuzo ikiwemo ya Wimbo Bora wa Kucheza wa
Mwaka (AFRIMMA), Mtumbuizaji Bora (MAMA), Msanii Bora wa Mwaka (MTV
EMA), Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (AFRIMA) na nyingine nyingi.
0 comments:
Post a Comment