Argentna ikipoteza mchezo wa fainali ya Copa America mbele ya Chile ‘La Roja’,hatimae mshambualiaji huyo wa Barcelona ameamua kuachana na timu yake ya taifa kwa kutangaza...
rasmi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina.
Baada ya game dhidi ya Chile, nyota huyo mwenye miaka 29 amekiambia kituo cha TYC Sports kwamba, amaisha yake ya soka la kimataifa yamefika mwisho.
“Kwasasa timu ya taifa basi tena. Baada ya kupoteza fainali nne sitaendelea tena kuitumikia timu ya taifa. Naamini tayari maamuzi yameshafanyika. Nimechukua muamuzi huu kwa ajili yangu pamoja na watu wengu waliotaka iwe hivi.
Nimepambana sana, lakini ninaondoka nikiwa sijafanikiwa”.Alisema Messi mwenye umri wa miaka 29.
Video-Messi akitangaza uamuzi wa kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina.
Je Messi atabadili maamuzi yake? Au ndiyo basi tena na amemaliza maisha yake ya soka bila kushinda kombe la dunia,tusubiri tuone
0 comments:
Post a Comment