Msanii wa muziki na Mkurugenzi wa kundi la Radar Entertainment, TID
ameingia kwenye mgogoro na rapper Billnas aliyekuwa member wa kundi hilo
kabla ya kutimkia katika label mpya ya ‘LFLG’.
Mapema mwaka huu Billnas aliiambia Bongo5 kuwa aliondoka Rada bila matatizo na mtu yeyote. Akiongea na Clouds Fm, TID amedai Billnass amesahau alikotoka na hatoi...
heshima kwa watu walio msaidia kumfikisha hapo alipo sasa.
“Mi sijapenda alikuwa akinibembeleza nimsaidie ajulikane, alikuwa ana
nidhamu lakini sasa hivi hanipigii simu, tukimwambia afanye hivi
hataki,” alilalamika TID. “Why do we help people who do not help us, why
he think he is on top all over the sudden no!! People don’t live like
that… People need to respect the people who help u… And of the day,”
Aliongeza, “Mimi i gave out to my heart, my voice, my energy, my talent
to make him shine but I don’t see any effort, hajanipa hata laki moja
kuniambia nashukuru, anafanya tour hata kuniambia Mzee Mnyama chukua hii
laki tano umenifanyia chorus kali neve, huyo mtu wa aina gani hata
ungekuwa wewe usingefurahi basi hata shilingi elfu kumi. The first time
mimi ndiye niliyemleta Clouds Fm kufanya interview ananiambia siwezi
kuongea anatetemeka, ningetaka kumsign halafu ningemmaliza ingekuwa kila
napokwenda kufanya shoo angekuwa ananilipa lakini niliona kwamba sina
shida kitu nilichokuwa nakihitaji ni ‘appreciation’ ndo maana watu
wanatoa cirtificate of ‘Appreciation’,”
Kwa upnde wa Billnas akizungumzia issue hiyo alisema kuwa ameichukulia kawaida kauli hiyo na hajamkimbia TID.
“Mimi natambua mchango wake na nimewahi kuzungumza mara nyingi na najua
nafasi yake kwangu na sijawahi kumdharau na kuondoka Radar halitakiwi
liwe kosa,” alisema Billnass.
Saturday, June 25, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment