Muuza sura kwenye filamu za Kibongo, Hemed Suleiman
‘Hemed PHD’ amefunguka kuwa japo ni staa na mtu maarufu Tanzania lakini
hata siku moja hajawahi kufikiri kuwa atakuja kujihusisha kwenye
uhusiano wa kimapenzi na staa wa kike kutoka Bongo kwa sababu anafahamu
madhara yake.
dini yake ya Kiislamu inayomfanya aamini kuwa uhusiano ni suala binafsi ambalo halihitaji kushereheswa na watu.
“Unajua vyombo vya habari vinapofahamu kuwa unatoka na staa fulani vinaanza kukuandama wewe pamoja na huyo mpenzi wako. Si kitu kizuri kwa sababu mnapotofautiana pia vinaanza kuwazungumzia jambo ambalo wakati mwingine linaweza kusababisha hata msirudiane kutokana na misteki tu ndogo. So mimi sipendi kabisa maisha yangu yamulikwe ndiyo maana nimejiweka kando kwenye suala zima la uhusiano kutoka na staa,” alisema PHD.
0 comments:
Post a Comment