Thursday, June 30, 2016
VANESSA MDEE AELEZA WASI WASI WAKE JUU YA LEBO ZA MAREKANI NA AFRIKA
Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania wenye moyo mzito kila linapokuja suala la kusainishwa na label za nje. Ni kwasababu anaamini mfumo wa label za Kimarekani hauwezi kuzaa matunda kwenye...
muziki wa Afrika. Nilimuuliza of course, iwapo anaweza kusainishwa label, na haya ndio yalikuwa majibu yake:
Mfumo wa label Afrika ni tofauti kabisa, the concept of record label ilianzia nje, Marekani, Europe, Australia au nchi nyingine ambazo zinastructure kwenye industry. Sisi bado tunapigania mirabaha. So when you tell me a label inanisaidia, inanisaidia kwa kipi zaidi? Wananipa nini?
Labda nasaini distribution deal watanisaidia kusambaza muziki, great, labda wana nguvu za kunishinda mimi peke yangu. Lakini when you think of things the label supposed to do, I don’t know of any label in Africa, sijui.”
Ameongeza,”Nimekaa na wana Mavins, nimeangalia wanavyofanya kazi (akina Don Jazzy) at least naona kuna.. sio kutokana na nchi ya Nigeria na muziki wao, bali jinsi gani label inawahandle wasanii wao. So I can’t hate on it sababu sijawahi kuwepo kwenye label yoyote Afrika, but the way I see it, mimi pia nina wasiwasi.”
Amesema kama label ikimfuata imsainishe, bado atakuwa na wasiwasi.
“Of course ntakuwa najiuliza kwa kipi ambacho wananiongezea, kama ni mfumo wa Marekani it doesn’t work here, huku watu wanauza muziki barabarani so label zinatengeneza pesa kutokana na unit, how am I gonna pay back the money, it’s a difficult ball game. Unless waje na mfumo ambao unaweza kufanya kazi katika mazingira ya muziki wetu. Labda kama label itaniambia watalipia project, watanipa kiasi fulani cha fedha kufund project ya album kwa mfano na hiyo fedha itarudishwa kwa labda shows, endorsement or whatever, maybe it makes sense like that so that mimi situmii pesa za kwangu inakuwa kama loan kutoka kwa bank, sina uhakika na label za kwetu bado.”
Vanessa anaamini kuwa label zitakazoweza kufanya vizuri Afrika ni zile zilizoanzishwa na watu wenye uelewa wa muziki wa Afrika na jinsi unavyoingiza fedha. “Kuna kipindi nilikuwa naongea na Reekado Banks alikuwa anajitayarisha kutoa wimbo, nikamuuliza are you gonna sell it digitally? akasema ‘sisi hatufanyi hivyo, muziki tunatoa bure’ walisema label yetu haiamini hiyo structure, haifanyi kazi Afrika.”
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment