Pages

Subscribe:

Thursday, June 30, 2016

HADITHI: NYUMA YA MACHOZI (sehemu ya kumi na moja) 11


MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
ILIPOISHIA:
“Sawa,” Kinape aliitikia huku akimshika mkono Happy aliyekuwa ameiva na kuwa mwekundu kwa hasira. “Hebu ngoja,” Happy alijitoa mkononi mwa Kinape. “Happy hebu msikilize mwenzako,” Kilole aliingilia kati baada ya kuona Happy akitafuta msaada kwake. “Sikiliza dada, Kinape ananinyanyasa sana.” “Mdogo wangu ngoja nizungumze na mgeni, tutalimaliza nina imani kabisa Kinape anakupenda sana.” Kinape na Happy walitoka nje na kuwaacha Kilole na Jimmy.
SASA ENDELEA...


Usiku baada ya kutoka kumpiga picha za aibu Kilole, Jimmy alikuwa mtu mwenye mawazo mengi sana. Toka aanze kazi ile hakuwahi kukutana na tukio zito kama lile, Tokio kubwa lilikuwa...

kuwapiga picha za utupu wake za watu au mastaa wa kike. Lakini la kushuhudia mtu akifanya mapenzi lilikuwa ndilo tukio lake la kwanza lililompa wakati mgumu sana. 

Alitamani bora Kilole angempa penzi yeye kuliko kufanya mapenzi na mtu aliyekuwa sawa na maiti asiyejielewa. Alijikuta akipata maswali yasiyo na majibu juu ya kitendo cha Kilole kufanya mapenzi na mtu anayemfahamu ni shemeji yake. Alijiuliza kufanya tukio lile huku akipiga picha alikuwa na maana gani, alijikuta akiingiwa na tamaa ya mapenzi kwa kuamini kupitia picha zile lazima na yeye ataweza kumtia mikononi. 

Wazo lingine lilikuwa kutengeneza pesa zaidi kupitia picha zilezile. Baada ya kuwaza sana akiwa amejilaza kitandani alijikuta akitabasamu baada ya kugundua picha zile zitakuwa sawa jiwe moja kuua ndege wawili. Hakuamini kabisa mwanamke yule pamoja na kumtisha anaweza kumfanyia lolote baya. Kabla ya kulala alirudia kuangalia picha moja moja ili aone zipi zimetoka vizuri na zipi zimeharibika, alijikuta akiwa amepiga picha chache zenye ubora. Kutokana kupatwa na kigagaziko kilichomfanya aifanye kazi katika wakati mgumu. Picha zingine alipiga ukuta badala ya watu, zingine aliwapiga mgongo au kupiga sehemu isiyohusika. Zote ambazo zilikuwa hazifai alizifuta na kubakiza chache ambazo zilikuwa zinafaa. 

Baada ya kuwaza sana alipitiwa na usingizi mpaka siku ya pili, asubuhi alipoamka baada ya kuoga alikwenda studio kusafisha picha zake. Kama kawaida picha zake za magumashi zilikuwa zinawahishwa kusafishwa kabla hawajaanza kazi yoyote. “Beka kama kawaida piga mara mbili.” “Za nani mwana?” “Kaka aina haja ya kujua, nifanyie kazi haraka.” Beka alimsafishia Jimmy picha mara mbili na kumpatia, alizichukua na kurudi zake nyumbani kwanza kabla ya kuzipeleka kwa mwenyewe. Alipofika alipitia picha moja baada ya nyingine, alichukua za kwake na kuziweka kwenye kabati na zilizobaki alimpelekea Kilole.

Jimmy alipofika kwa Kilole alishtuka kumkuta Kinape nusra atimue mbio kwa mshtuko, lakini alificha hofu yake na kuingia ndani. Baada ya Kinape na mpenzi wake kutoka nje walibakia wawili ndani. “Karibu ukae,” Kilole alimkaribisha Jimmy baada ya kuonesha wasiwasi, alijua baada ya kumuona Kinape. “Asante,” alijibu huku akikaa, kutokana na wasiwasi walijikuta akikaa chini. “Jimmy mbona unanitia aibu kazi utaiweza kweli?” “Samahani, unajua nimeshtuka sana.” “Hajui lolote, wasiwasi wako tu.” “Mmh! Nilishtuka sikutegemea kumkuta.” 

“Tuachane na hayo mzigo wangu upo wapi?” Kilole aliuliza. Jimmy alimpa bahasha ya picha, baada ya kuipokea aliichukua na kwenda nayo chumbani. Hakutaka kuzipitia alichukua kiasi cha fedha alizobakia kwenye deni lao, alipofika sebuleni alipa fedha yake na kumwambia: “Nina imani kila kitu kimekwenda vizuri?” “Nashukuru.” “Jimmy kama kuna kitu chochote nitakueleza.” “Hakuna tatizo.” “Naomba siri hii usimwambie yeyote ikivuja nitajua ni wewe, kwa hiyo usinilaumu kwa lolote litakalokukuta.” “Kwangu shaka ondoa, hakuna kitu kama hicho.”

“Nakuhakikishia baada ya muda tegemea zawadi kubwa.“ “Nitashukuru sister.” “Basi baadaye.” Jimmy aliagana na Kilole na kuondoka zake, baada ya kuondoka Kilole alitoka nje na kuwakuta Kinape na Happy wakiwa katika mazungumzo ya kawaida. “Vipi jamani?” “Yamekwisha,” alisema Kinape. “Basi niwaache mimi nipo ndani.” “Hakuna tatizo.” Kilole alirudi ndani na kuingia chumbani kuangalia picha alizoletewa na Jimmy. Baada ya kufungua bahasha alichukua alitoa picha zote na kuzimwaga kitandani na kuanza kupitia picha moja baada ya nyingine. 

Zilikuwa picha za aibu ambazo hazikuonesha uhalisia wa watu wawili waliokuwa wanafanya mapenzi kwa ushirikiano. Picha zile zingekuwa kwa upande wa pili kwa ajili ya kumdhalilisha zingekuwa nzuri sana. Lakini kama mtego wa kuonesha wanafanya mapenzi alikuwa amefeli. Alijiuliza kama Kinape angegoma kufanya naye mapenzi, picha zile zisingeweza kumshtua kwani ilionesha wazi hakukuwa na ushirikiano wowote wa Kinape kwake. 

Moyoni alishukuru mkwala wake uliweza kumlainisha lakini kama angetegemea picha zile zisingemsaidia. Alijikuta akipandwa na hasira na kuamua kuzichana zote kisha aliziweka kwenye chombo na kuzichoma moto. Baada ya kuzichoma moto aliamini pamoja na kumtega na kuweza kufanya naye mapenzi bado hawezi kumdhibiti Kinape kwa vile ana uwezo wa kukataa na asimfanye lolote. Wazo lingine lililomjia ni kufanya naye tena mapenzi huku Jimmy akipiga picha wote wakiwa na akili timamu. 

Aliamini kwa mpango ule ataweza kumdhibiti Kinape pia hata kuweza kuvunja penzi lake na Happy ambalo kila kukicha lilimnyima raha. Alijikuta akijilaumu kwa kupanga mpango mbovu, lakini kwa upande mwingine ulisaidia kuweza kumvuta karibu Kinape mpenzi wake wa zamani. Alitoka nje na kuwakuta Kinape na Happy sebuleni wakizungumza, walipomuona waliacha kuzungumza na kumwangalia.

Uso wa Kilole ulionesha kuna kitu kimemsibu. Kinape alijua ni kutokana na Happy kuwa pale. “Dada vipi, bado unamkumbuka shemeji?” “Aah, wapi mbona nimeishazoea.” “Shemu vipi?” Kinape aliuliza. “Nikuone mara moja.” “Hakuna tatizo,” Kinape alijibu huku akinyanyuka. Kilole na Kinape walisogea pembeni, Kinape alijua lazima atagombezwa kuhusu Happy. 


“Kinape, kwanza samahani kwa kukukatisha kazungumzo na mpenzio.” “Bila samahani.” “Nina ombi moja, leo naomba tulale pamoja, kesho endelea na mpenzi wako.” “Hakuna tatizo.” “Basi endeleeni ma mazungumzo yenu.” Kinape alishangazwa na ustaarabu alioonesha Kilole, lakini moyoni alipanga Deus akirudi lazima aondoke. Kilole alifurahia kukubaliwa ombi lake bila masharti yoyote, alimpigia simu Jimmy kumjulisha kazi nyingine ya usiku ule. “Jimmy.” “Ooh! Sister lete mpya.”
”Ile kazi haikuwa nzuri nataka leo tuirudie.” 


“Kwa malipo yaleyale?” “Hapana, nitakupa laki na nusu.” “Poa, nije saa ngapi?” “Saa mbili usiku, ila ukifika usiingine ndani nipigie simu, ooh! Nimekumbuka hebu njoo mara moja,” Kilole alikumbuka kazi ile ilitakiwa ifanyiwe maandalizi ili isije kwenda kinyume kutokana na muda wa kurudi mumewe kuwa umekaribia. Wakati huo Kinape na Happy walikuwa wameondoka na kuahidi kurudi jioni. Baada ya muda Jimmy alifika, alimzungusha kwa nyuma sehemu ya dirishani ili kuandaa maandalizi ya kupiga picha za ndani. 

Baada ya kuandaa eneo vizuri waliagana na kukubaliana kukutana muda huo. Majira ya saa mbili usiku Kinape alikuwa nyumbani, baada ya chakula cha usiku walikwenda chumbani kulala. Kama kawaida Jimmy alikuwa amekwishafika eneo la tukio. Baada ya kupewa taarifa ya kuacha kwa mchezo mchafu, alisogea dirishani na kuchungulia ndani. Ili kupata uhakika kama Jimmy amefika alinyanyuka na kwenda dirishani kama anataka kusogeza pazia, alipoangalia nje alimuona. Alilidhika na kurudi kitandani kuendelea na zoezi lake. Naye Jimmy kama alivyoelekezwa alipiga picha kutokana na jinsi Kilole alivyokuwa akifanya bila Kinape kujua. 

Japo alikuwa kwenye wakati mgumu huku akijawa na mawazo mtu na shemeji yake kufanya mapenzi. Hakutaka kujua sana, lakini katika siku iliyokuwa ngumu kwake ilikuwa ile. Mpaka wanamaliza Jimmy alikuwa hoi na kujichafua kutokana na kwenda na muvu ya mchezo. Baada ya kumaliza mpango wake Kilole alimtanguliza Kinape bafuni na yeye kutoka nje kuonana na Jimmy. “Vipi umefanikiwa?” Kilole alimuuliza Jimmy baada ya kumuona.

 “Ndiyo.” “Hebu nione.” Jimmy alimuonesha picha alizopiga katika hatua zote, zilikuwa picha nzuri sana ambazo aliamini kama Jimmy akiziona hawezi kuruka. “Jimmy kazi nzuri.” “Lakini umenipa mateso makubwa.” “Pole nitakuongezea elfu hamsini kwa hiyo itakuwa lakini mbili. Shika laki mbili zingine kesho.” “Hakuna tatizo, kuna lingine?” “Hakuna.” “Basi kesho.” Waliagana kwa Kilole kurudi ndani huku moyo wake ukiwa na furaha, alijikuta akiingia chumbani huku akitabasamu. “Vipi mbona una furaha?” Kinape alimuuliza. 

“Leo umekumbusha mbali sana.” “Umekumbuka nini?” “Penzi letu lilivyokuwa tamu adhimu, hakika leo nitalala usingizi mtamu.” “Lakini kumbuka kitendo hiki ni sawa na kukata tawi tulilo kalia.” “Hii ni siri yetu.” “Hakuna siri katika mapenzi.” “Basi kwetu itakuwa siri.” “Nimefanya tu lakini si kwa moyo wangu.” “Kinape mbona unataka kutia mchanga kwenye chakula kitamu, kwa vile tumeamua kula nguruwe basi tumchague aliyenona.” “Kumbuka mwenyewe muda si mrefu atakuwa hapa.” “Tutakuwa kama hatujuani, ila siku tukipata nafasi kama kawaida.” Waliendelea kula raha zao mpaka siku ya pili, huku moyoni Kilole akiapa akifanikiwa kuzipata picha zile lazima Kinape arudi mikononi mwake na kuvunja uchumba wake Happy.

Jimmy baada ya kufika kwake alijikuta akizidi kuwa na maswali mazito juu ya kitendo cha Kilole na Kinape kumhujumu Deus. Lakini bado alikuwa wazo lake la kuhakikisha kupitia picha zake anampata kimapenzi. Aliamini kama angekuwa na kamera ya kuchukua video basi angepata mkanda ambao angeweza kuuza kwa fedha nyingi siku za mbele. Pia aliona kupitia picha zile angepata faida mara mbili, hakuwa na haja ya kuzichambua kwa vile alizipiga katika ustadi mkubwa. 

Aliweka kamera yake kwenye kabati na kutoka nje kwenda kutafuta mwanamke wa kulala naye kwani alikuwa kwenye hali ngumu. Jimmy aliposhtuka siku ya pili alijikuta peke yake kitandani, mwanamke aliyelala naye hakuwepo. Hakujishughulisha naye baada ya kuoga aliwahi kusafisha picha, alimkuta Beka na kumweleza amsafishie mara mbili kama kawaida. Baada ya kusafishiwa alizichukua na kuzipeleka nyumbani, alipofika alishangaa kukuta sehemu alipoweka picha alizompiga Kilole mara ya kwanza hazipo. 

Kilichomshangaza ufunguo wa chumba chake alikuwanao mwenyewe. Alijikuta akishtuka na kujiuliza nani aliyechukua. Alikumbuka changudoa aliyelala naye na kuondoka akiwa amelala ndiye aliyechukua zile picha, alijiuliza amezichukua ili iweje. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kama zikivunja lazima Kilole atamuona hana manaa hata kumfanyia kitu kibaya.
Alipanga usiku akamtafute ili amrudishie picha zake, alichukua picha alizosafisha na kumpelekea Kilole.
 

Itaendelea...

0 comments:

Post a Comment