skip to main |
skip to sidebar
SNURA: WIMBO WA MAJANGA ULINIPA MAJANGA
STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Snura Mushi ambaye alipata kiki ya
aina yake kwa kibao chake cha Majanga, amefunguka kuwa licha ya kupata
shoo nyingi kupitia ngoma hiyo, lakini pia alipata majanga kwa
kutapeliwa mara kadhaa. Akipiga, Snura alisema promota mmoja alimpeleka
kufanya shoo mkoani Kilimanjaro na Mererani Arusha, lakini baada ya
kuwa ameshafanya kazi, mtu huyo...
alimkimbia bila kumpa chake, kiasi
kwamba alilazimika kurejea Dar kwa lifti.
“Sitasahau, nilisaidiwa lifti mimi na wacheza shoo wangu kutuleta
Dar, lakini baadaye nilikuja kumpata huyo promota, nikamnyang’anya pete
ya ndoa na uchumba, ninazo mpaka leo maana hakunilipa,” alisema Snura.
0 comments:
Post a Comment