Paparazi aliyekuwa akifanya ziara ya kushtukiza mara kwa mara back stage, kuna wakati alifanikiwa kumkuta Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa... ushirikiano.
“Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.
Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Baraka, Linah alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.
“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.
Kwa upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.
0 comments:
Post a Comment