Muandaaji wa nyimbo za bongo fleva nchini, Emma The Boy amewataka
ma-producer kuacha njaa ili waweze kupata heshima kama anavyopata
'producer' mkongwe Master J.
Emma
amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV baada
ya kuwepo madai ya wasanii wa bongo fleva kutokuwa na nidhamu kwa
watarishaji wao wa muziki kwa kile wanachosema kuwa...
msanii
akishatengenezewa 'hit song' huwa hawakumbuki tena mtayarishaji wake
wala hata kumpa sifa zake pindi awapo katika mahojiano na vyombo vya
habari.
"Ma-producer sisi wenyewe
tuna tabia ya njaa, njaa zimezidi. Msanii anakuja na Laki moja au elfu
sabini au elfu hamsini kwa sababu ya njaa zako unatengeneza kitu kwa
msanii ambaye hana uwezo wa kufanya hivyo. Kwa hiyo mbeleni lazima
ikushushe kwa sababu msanii hakuimba kwenye kiwango chake kwa hiyo
inakushusha wewe hata kama ulikuwa na ukubwa gani unakosa hiyo heshima", amesema Emma the boy.
Kwa upande mwingine, Emma amewakumbusha
wasanii watambue kuwa ma-producer ndiyo kila kila kitu kwa wasanii kwani
nyimbo yako ikiwa mbaya haitaweza kufika kokote pale.
0 comments:
Post a Comment