Tuesday, July 18, 2017
STORY: KAHABA KUTOKA CHINA (Sehemu ya kwanza) 01
“Nisikilize Rose. Unataka niseme nini ili ujue kwamba nakupenda? Unataka nifanye nini ili ujue kwamba nakuhitaji? Au unataka nijiue? Au unataka usikie nimekimbizwa hospitali baada ya kunywa sumu ya panya kwa lengo la kujiua kwa sababu umenikataa? Naomba unionee huruma, naomba uone ni kwa jinsi gani umekuwa wa thamani kwangu. Naomba unielewe mrembo, ninakupenda sana.”
“Hivi Rose! Malkia wa moyo wangu hebu niambie nikwambie nini ili unielewe. Au mpaka niseme kwamba ninakupenda zaidi ya mama yangu? Au mpaka...
niseme kwamba ninakupenda zaidi ya ninavyojipenda? Hebu niambie nikwambie nini mtoto wa kike.
Usifikiri kwamba nimekuona na kukutamani tu, nimekupenda toka moyoni mwangu na hata kama utakuwa tayari nifike hapo kwenu na kukutolea mahari ili nikuchukue jumla hebu niambie ili nije. Naomba unijibu, jibu lako zuri ndio litakuwa faraja ya moyo wangu usiku wa leo. Nakupenda mrembo”
Hizo zilikuwa meseji miongoni mwa meseji ambazo Rose alikuwa ametumiwa usiku wa siku hiyo, zilikuwa ni meseji ambazo zilitumwa na watu ambao walikuwa wameangukia katika penzi la msichana Rose ambaye kwao alionekana kuwa kama msumbufu. Kila siku Rose alikuwa msichana wa kupokea meseji kutoka kwa wavulana mbalimbali ambao walikuwa wakimtaka kimapenzi. Rose hakuonekana kuwa mwepesi kukubaliana nao, kwake, aliwaona wanaume kuwa wadanganyifu ambao walikuwa wakitaka kumchezea na kisha kumuacha katika mataa akilia.
Uzuri wake ndio ambao ulikuwa ukiwavutia wavulana wengi ambao walikuwa wakipanga mstari na kisha kumfuatilia Rose kila alipokuwa akienda nje ya nyumba yao. Alipokuwa akielekea dukani, alikuwa akipata wasindikizaji, alipokuwa akielekea sokoni napo alikuwa akipata wasidikizaji ambao kazi yao ilikuwa ni kumbebea kapu la mboga mpaka anafika nyumbani kwao.
Wavulana wa mtaa wa Magomeni Mapipa wakaonekana kuchanganyikiwa na uzuri wa Rose. Uso wake mwembamba, umbo lake la kimiss, hipsi zake ambazo zilikuwa zimetokeza kidogo kama za pundamilia unapomtazama kwa nyuma, tumbo lake lililoingia ndani pamoja na vijishimo viwili mashavuni vilivyokuwa vikionekana kila alipokuwa akicheka au kutabasamu ndivyo ambavyo vilikuwa vitu ambavyo viliwavutia wavulana wengi ambao walikuwa wakimwangalia.
Rose alionekana kama anafanya kusudi, kila alipokuwa akipita mbele ya wanaume, mwendo wake ulikuwa ni wa mapozi kana kwamba hakuwa akikanyaga ardhi hii ambayo watu walikuwa wakiitumia kuchimba vyoo, kila alipokuwa akipita karibu na wanaume, alikuwa akitoa tabasamu ambalo lilikuwa likiwavutia wavulana wengi kumwangalia kwa matamanio.
Rose hakuwa mwepesi hata kidogo, Rose hakuonekana kuwakubalia wanaume ambao walikuwa wakimwambia maneno mengi ya kimapenzi, kwao, Rose alionekana kuwa kama muuaji kwani hata kama ulikuwa ukiongea huku machozi yakikutoka, Rose hakukuonea huruma, alikuwa akiamini sana katika msemo wa ‘ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni’.
Wavulana wa Magomeni Mapipa walikuwa wamepanga foleni lakini hakukuwa na mtu ambaye alifanikiwa kumpata Rose ambaye sifa za uzuri wake zilikuwa zikienea kwa kasi sana kila siku masikioni mwa watu. Vijana wengine ambao walikuwa wakikaa Magomeni Mikumi na sehemu nyingine walikuwa wakifika Mapipa kwa ajili ya kumuona Rose tu ambaye alikuwa akitikisa sana katika miaka hiyo.
Rose hakuonekana kuwa mtu wa hasira, kila alipokuwa akitongozwa, tabasamu pana lilikuwa likionekana usoni mwake, tabasamu ambalo lilimpa faraja kila mwanaume ambaye alikuwa akijaribu bahati yake ila tatizo lilikuwa moja tu, jibu lake alilokuwa akilitoa lilikuwa tofauti na tabasamu lile jambo ambalo lilionekana kuwashangaza wavulana wengi.
Rose alikuwa binti pekee wa mzee Shedrack, mzee ambaye alikuwa mwanajeshi ambaye kambi iliyokuwa Lugalo. Mzee Shedrack alijua fika kwamba binti yake, Rose alikuwa msichana mzuri ambaye alikuwa na mvuto mkubwa kwa kila mwanamume ambaye alikuwa akimwangalia, alichokifanya yeye ni kumpa tahadhari juu ya kila uamuzi ambao alikuwa akiufanaya kuhusiana na wanaume ambao walikuwa wakimfuata kila siku.
Rose alionekana kuwa muelewa, kila wakati maneno ya baba yake yalikuwa yakijirudia kichwani mwake. Maneno yale yakamfanya kutokutamani wanaume, maneno yale yakamfanya kuwachukia wanaume na kuwaona kwamba wote walikuwa wadanganyifu. Maneno yale ya baba yake ndio yalikuwa chachu kubwa katika maisha yake, yalikuwa maneno ambayo yalimpa nguvu kubwa ya kumkataa kila mwaume ambaye alikuwa akisimama mbele yake kumtongoza.
Pamoja na hayo yote, ukali wa baba yake ulikuwa ukimuogopesha kupita kawaida. Mikanda ambayo ilikuwa ikitumika kumchapa katika kipindi cha nyuma ndio ambayo ilimfanya kumuona baba yake kutokuwa na masihala hata kidogo. Mikanda ile ndio ambayo ilimfanya kusimama mbali na wanaume ambao alikuwa akiongea nao kwa ajili ya kumuogopa baba yake ambaye alikuwa mkali kupita kawaida.
Wanaume wengi ambao walikuwa wakimfuatilia Rose walikuwa wakipigwa na mzee Shedrack ambaye alionekana kuwa katili mtaani pale. Japokuwa vijana walikuwa wakipigwa sana na mzee huyo lakini hakukuwa na mvulana ambaye alionekana kukata tamaa kumfuata Rose, msichana huyo bado alikuwa chaguo la kila mvulana ambaye alikuwa akimwangalia.
Siku ziliendelea kukatika na mwisho wa siku wasanii wakubwa wa muziki na maigizo kuanza kumnyemelea Rose. Mtu wa kwanza kabisa ambaye alikuwa maarufu kuanza kumnyemelea Rose alikuwa msanii wa muziki ambaye katika kipindi hicho alikuwa juu sana, Yusufu au The Ruler kama ambavyo alikuwa akijulikana na wengi.
Yusufu alikwenda kwa kujiamini sana, jina lake lilikuwa likimpa kiburi kwa kujiona kwamba angempata Rose lakini mwisho wa siku akajikuta akimaliza soli za viatu kwa kutembea kutoka Kijitonyama mpaka Magomeni pasipo kufanikiwa kumpata msichana huyo.
Watu hawakuishi hapo, mtu wa pili kumfuata Rose alikuwa mwandishi wa hadithi ambaye alikuwa akivuma sana nchini Tanzania kwa wakati huo, Andrew Carlos. Nae alijaribu sana kumfuata Rose, alitumia kila njia ya kumpata Rose, alilitumia sana jina lake katika vitabu vyke vya hadithi pamoja na kuwaambia watu dhahiri kwamba alikuwa akimpenda Rose lakini mwisho wa siku akajikuta akipoteza muda wake kwa ajili ya kumfuatilia msichana huyo.
Rose hakuonekana kuwa mwepesi hata mara moja, alijua fika kwamba kulikuwa na wanaume wengine walikuwa wakimpenda kwa moyo mmoja lakini bado hofu ilikuwa kubwa kwa baba yake. Alikuwa akimuogopa sana baba yake ambaye mara kwa mara alionekana kuwa kama muuaji mbele ya macho yake.
Ukiachana na Rose, mzee Shedrack alikuwa na mtoto mwingine wa kiume, huyu aliitwa John. John alionekana kuwa kama mlinzi katika maisha ya Rose, mara kwa mara yeye ndiye ambaye alikuwa akimpelekea kesi baba yake kuhusiana na Rose. Kila alipokuwa akimuona kasimama na mwanaume, John alikuwa akimfikishia taarifa baba yake ambaye alionekana kuwa kwenye hasira kali.
“Kuna siku nitakuua wewe malaya wa kike,” Mzee Shedrack alimwambia Rose huku akionekana kuwa na hasira.
“Wao wananitaka baba….mimi nawakataa,” Rose alijitetea huku akilia.
“Hata kama. Yaani kila siku wakutake wewe tu, yaani kila siku wakusimamishe wewe tu. Nitakuua. Rose nitakuua. Wewe ngoja ulete mimba humu ndani. Nitakuua. Narudia tena, NITAKUUA,” Mzee Shedrack alimwambia Rose huku akionekana kuwa na hasira mpaka mishipa ya shingo ikasimama.
Kila siku maisha ya Rose yalikuwa ya hofu, maneno makali ambayo alikuwa akiongea baba yake kila siku yalimuogopesha. Katika kipindi hicho hawakuwa wakiishi na mama yao kwani alikuwa amefariki miaka mitatu iliyopita huku tetesi zikisema kwamba mzee Shedrack ndiye aliyemuua kutokana na wivu wa mapenzi, kifo ambacho kilikuwa na utata mkubwa.
Hayo ndio yalikuwa maisha ya Rose, kila siku wanaume walikuwa wakijileta kwake, hakutaka kuwapa nafasi, baba yake alionekana kuwa makini sana katika maisha yake. Rose akawa mtu wa kuwakatalia wanaume kila siku. Japokuwa alikuwa amevunja ungo, kuwa na matamanio kama wanawake wengine lakini hakuweza kuwa na mwanaume yeyote kwa ajili ya kukidhi tamaa ya mwili wake, sababu kubwa ni kwamba alikuwa akimhofia baba yake.
Kila siku Rose alikuwa mtu wa kushinda ndani, mzee Shedrack akaendelea kumuweka John kuwa mlinzi wa dada yake. Kila siku ambazo Rose alikuwa akitoka ndani ya nyumba, John alikuwa akimfikishia baba yake taarifa, alipokuwa akirudi, ilikuwa ni kama vita ndani ya nyumba mpaka pale alipoeleza sababu iliyomfanya kutoka ndani ya nyumba hiyo.
Maisha yaliendelea kuwa hivyo kila siku, Rose hakuonekana kuwa na amani kabisa nyumbani kwao. Japokuwa katika kipindi hicho alitakiwa kuanza kidato cha tano lakini baba yake hakuwa tayari kumpeleka shule binti yake, kila siku alikuwa akimtaka kubaki ndani ya nyumba hiyo hiyo. Kitendo hicho ndicho ambacho kilianzisha mawazo mengine kichwani mwa Rose kwamba baba yake alikuwa akimtaka kimapenzi na ndiyo maana hakumpa hata nafasi ya kutoka ndani ya nyumba hiyo.
Mawazo hayo yaliendelea kuwepo ndani ya kichwa chake lakini kila siku alikuwa akiyapuuzia tu kwa kuyaona ni mawazo machafu ambayo yalikuwa yakipandikizwa na shetani kichwani mwake. Mara kwa mara alipokuwa chumbani kwake, Rose alikuwa na tabia ya kusimama mbele ya kioo na kisha kuanza kujiangalia, alikuwa akiliona umbo lake kuvutia kupita kawaida, kifua chake na sura yake nzuri vilikuwa vitu ambavyo vilimvutia kupita kawaida.
“Mtoto wa shangazi yako atakuja hapa. Nataka ukae naye kwa amani na huo umalayamalaya wako uuache, usinitie aibu,” Mzee Shedrack alimwambia Rose.
“Nani?”
“Irene. Anakuja kwa ajili ya likizo ya chuoni kwao. Nakuomba umuonyeshee upendo wote. Umenisikia?”
“Nimesikia baba,” Rose alimjibu baba yake.
Baada ya siku mbili, msichana Irene akafika nyumbani hapo. Kama alivyokuwa Rose, Irene naye alikuwa mrembo sana. Umbo lake lilikuwa la mvuto sana, makalio yake yalikuwa makubwa jambo ambalo lilimfanya kujivunia kila alipokuwa akijiangalia katika kioo. Kwa muonekano tu, Irene alionekana kuwa msichana mtulivu sana, uso wake ulikuwa ni wa upole.
Usingeweza kujua kwamba ile sura ilikuwa ni kama kinyago tu kwani maisha yake ya nyuma ya pazia yalikuwa mabaya, maisha ambayo kusingekuwa na mzazi yeyote ambaye angetamani msichana Irene kukaa pamoja na binti yake.
Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Irene alionekana kuwa msichana mpole ambaye alikuwa akiwaponda wanaume kila siku mbele ya mjomba wake jambo ambalo lilimfanya Mzee Shedrack kumsifia kila siku na kumtaka Rose kuiga maisha yale na si kila siku kusimama na wanaume njiani.
“Umemuona mwenzako. Hawapendi kabisa wanaume na si kama wewe. Kila siku ni kusimama na wanaume tu njiani. Narudia tena. Siku ukipata mimba, bora utafute pa kwenda,” Mzee Shedrack alimwambia Rose huku akimsisitizia kwamba ilikuwa ni lazima awachukie wanaume.
Irene ndiye aliyekuwa karibu naye sana katika kipindi hicho, ndiye aliyekuwa rafiki yake mkubwa ambaye alikuwa akiishi naye karibu yake kila siku. Mara kwa mara walikuwa wakielekea sokoni pamoja na kurudi nyumbani. Kwa wanaume, wakachanganyikiwa kwa Irene, makalio yake makubwa yakawadatisha mno.
“Mmmh! Una umbo zuri Irene,” Rose alimwambia Irene ambaye alikuwa amesimama akiwa mtupu mbele ya kioo.
“Asante shosti. Ila mbona na wewe una umbo zuri sana,” Irene alimwambia Rose.
“Hapana. Umbo langu wala siyo zuri kama lako. Hebu niangalie,” Rose alimwambia Irene huku akisimama.
“Una umbo zuri sana. Hebu jaribu kuvua nguo zako uone,” Irene alimwambia Rose ambaye akaanza kuvua nguo na kubaki mtupu.
“Hebu jiangalie Rose. Unavutia,” Irene alimwambia Rose huku akiwa amemsogelea. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa ameanza kukifanya ni kukipeleka kinywa chake katika kifua cha Rose.
Rose akashtuka, hakuamini kama Irene angeweza kumfanyia kitu kama kile, alitaka kumtoa, lakini kila alipotaka kufanya hivyo, alijisikia kuwa katika hali ambayo hakuwahi kuwa nayo kabla.
Irene hakuishia hapo. Bado aliendelea vile vile kuuchezea mwili wa Rose mpaka pale ambapo alianza kumuona Rose akianza kuchanganyikiwa na yeye mwenyewe kukifuata kitanda na kulala. Irene hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kuelekea katika mkoba wake na kisha kutoa kitu ambacho kilikuwa kwenye karatasi.
“Nini hicho?” Rose aliuliza huku sauti yake ikiwa imebadilika.
“Kiungo cha bandia” Irene alimjibu huku akimsogela pale kitandani.
“Unataka kufanya nao nini?”
“Kwa ajili yako Rose. Unapokuwa na huu, hata hamu ya mwanaume unakuwa hauna,” Irene alimwambia Rose ambaye alishangaa.
“Hapana. Haiwezekani. Sitaki Irene. Haiwezekani” Rose alimwambia Irene.
“Kwa nini?”
“Sijawahi kufanya mapenzi.”
“Hilo si tatizo. Tena wewe ndiye mtu mzuri. Usimfanye mwanaume kuimwaga damu yako kitandani. Wengi wanakuwa makatili, hawaoni hata huruma,” Irene alimwambia Rose kwa sauti ya chini.
“Hapana. Haiwezekani,” Rose alimwambia Irene huku akisimama na kisha kuanza kuvaa nguo zake.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane hapahapa.
Labels:
HABARI & UDAKU,
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment