Msanii Alikiba ambaye ni shabiki wa klabu ya Yanga, amesema haiogopi
wala kuihofia timu ya Simba hata kama wameanza vizuri kwa kugawa
kichapo katika mechi za awali Ligi Kuu huku akidai mpira unadunda na
muda wowote Simba itapotea.
Alikiba
ameeleza hayo muda mchache alipomaliza mahojiano kwenye kipindi
cha Planet Bongo akiwa ameongozana na
mtayarishaji wake...
wa wimbo mpya wa 'seduce me', Man Water ambao kwa sasa
unazidi kuwa gumzo katika mtandao wa 'Youtube' kwa kufika watazamaji
Milioni mbili.
"Simba hainitishi, Simba
anafungiwa bandani ndiyo nimuogope mimi ?, kama kawapiga 7-0 Ruvu
Shooting ni vijana wengine sisi hatuna shida japo ametufunga katika
mechi ya watani wa jadi lakini hiyo ni kawaida na ndiyo maana ukisikia
mpira unadunda maana yake ni kwamba mchezo unabadilika", alisema Alikiba.
Pamoja na hayo Alikiba aliweza pia
kuzungumzia sakata la kuondoka kwa mchezaji ambaye alikuwa anampenda kwa
umahiri wa kulisakata kabumbu ambaye ni Haruna Niyonzima katika timu
yao na kwenda Simba.
"Sidhani kwa kuondoka kwa
mchezaji Haruna Ninyozima katika klabu yetu kama itaweza kutuletea
madhara yoyote yale japo alikuwa ana kiwango kikubwa sana na
ninamkubali, lakini ninaimani tumepata vyuma vingine vyenye nguvu kama
vilivyoondoka ndiyo uzuri wa Yanga wana 'replace', ukibandua tu
tunabandika japokuwa klabu imeingiza mpunga hatuna shida", alisema Alikiba.
"Ninachowaombea Yanga wakaze
kwa kuwa naamini wana uwezo mkubwa sana na wachezaji wazuri sidhani
kama kuna mapungufu yoyote yakawadhohofisha wachezaji au wana Yanga
wakarudi nyuma. Sisi 'always' daima mbele hicho ndicho najua mimi", alisisitiza Alikiba.
Kwa upande mwingine, Alikiba amesema
haoni hatari yoyote kwa klabu yake kutoa sare ya bao 1-1 na timu ya
Lipuli FC mchezo uliyopigwa Agosti 26 mwaka huu katika mechi za ufunguzi
wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa bado Ligi haijanza kushika kasi huku
akijipa matumaini kuwa timu yake itakuja kufanya maajabu katika mechi
zijazo.
0 comments:
Post a Comment