Msanii wa bongo fleva na mkali wa R&B, Rama Dee amefunguka kwa
kuwataka vijana kuchangamkia fursa ya ajira inayotokana na mchezo wa
mpira wa kikapu ili waweze kuondokana na janga la utegemezi katika
familia pamoja na kujiinua kiuchumi.
Rama
Dee amebainisha hayo muda mchache alipowasili katika viwanja vya Don
Bosco Oysterbay JIjini Dar es Salaam, ilipokuwa...
ikifanyikia fainali za
Sprite BBall Kings 'game 4' baina ya TMT dhidi ya Mchenga BBall Stars na
kuwaomba wazee wawe tayari katika kuekeza katika michezo hasa mpira wa
kikapu ili uweze kusonga mbele zaidi kama walivyoamua kufanya uongozi wa
EATV pamoja na Sprite.
"Binafsi nawashukuru EATV
LTD kwa kushirikiana na Sprite kuweza kuupa kipaumbele mchezo wa
basketball kwa kuwa ulikuwa unapotea kabisa. Vijana sasa wanapaswa
waamke na kuchangamkia fursa iliyopo katika mpira wa kikapu kwa kuwa
inatoa ajira",alisema Rama Dee.
0 comments:
Post a Comment