Rapa Bill Nas ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya wa 'Sina
Jambo' amefunguka kwa kumtolea nje Nandy kwa kudai hajawahi kutoka naye
kimapenzi kama watu wanavyofikilia katika vichwa vyao kila kukicha.
Bill
Nas ameeleza hayo kupitia eNewz kutoka EATV baada ya yeye kuhusishwa
katika suala la kimapenzi na msanii wa bongo fleva Nandy na kusema hilo
jambo halina ukweli wowote hata...
watu wake wa karibu wanashangaa kusikia
hilo jambo.
"Siyo kweli, sijawahi
kuhusiana na msanii yoyote wa kike iwe wa bongo fleva au bongo 'movie'.
Mtu wangu wa mwisho niliyekuwa naye alikuwa ameajiriwa katika kampuni
binafsi. Mimi nipo 'single' hata watu wangu wa karibu wanaelewa hilo
halafu hizo stoti mimi nazisikia kutoka kwa watu wa mbali ", alisema Bill Nas.
Pamoja na hayo, Bill Nas amesema kwa
upande wake suala la mapenzi hawezi kulipa kipaumbele kama watu wengine
wanavyofanya kwa madai linampoteza 'focus' katika vile alivyovipanga
kuvitekeleza katika maisha yake.
0 comments:
Post a Comment