Tuesday, August 29, 2017
FAIDA 6 ZA KULALA BILA NGUO (UTUPU) NYAKATI ZA USIKU
Mara nyingi tumezoea kulala na nguo nyepesi ifikapo usiku, pia kuna watu wengine hujifunika mashuka au blenketi. Kwa mujiu wa makala mbalimbali za afya zinaeleza kuwa si vizuri kiafya kulala na nguo. Hizi ni faida chache za kuto lala na nguo nyakati za usiku.
1. Hutengeneza uhusiano mzuri ukisaidiwa na kichocheo cha Oxytocin.
Natasha Turner, daktari wa...
tiba asilia aliyeandika kwenye blogu ya Huff Post Canada, alifichua kwamba kulala karibu au mkiwa mmekumbatiana na mwenzi wako mkiwa bila nguo hufanya mwili kutoa kichocheo kiitwacho Oxytocin kinachofanya ujisikie vizuri.
Hii inatokea pale kunapokuwa na mgusano wa ngozi kwa ngozi, hii inaweza kusaidia kuondoa msongo (Stress) na kushuka moyo (Depression). Oxytocin pia inaweza kupunguza shinikizo la damu, kuimarisha tumbo na kupunguza uvimbe kwenye utumbo. Pia, utendaji wako wa tendo la ndoa pengine unaweza kuboreka.
2. Hukufanya ubaki kijana.
Inashauri kuweka mwili katika jotoridi chini ya 21°C ukiwa kitandani na njia nzuri kufanya hivyo ni kulala uchi/mtupu. Hii huruhusu vichocheo vinavyozuia uzee na Melatonin ambayo hudhibiti mzunguko wa kusinzia na kuamka kutenda kazi vizuri. Utajihisi huru, Kulala kitandani kwako, bila kuvaa chochote inakufanya kujisikia huru.
3. Huhamasisha vichocheo vya furaha.
Unapolala na nguo au kulala chini ya blanketi zito unazuia utokaji wa kichocheo cha ukuaji (Growth Hormone/HGH). Hii ina maana hutoweza kupunguza mafuta ukiwa katika usingizi au hautofaidika na ukarabati wa usiku wa mifupa, ngozi na nyama za mwili wako.
Kulala uchi/mtupu pia huthibiti kiwango cha Cortisol, zinazo dhoofisha kinga ya mwili, kupandisha shinikizo la damu na lehemu (Cholestrol), kuvuruga mpangilio wa usingizi, kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kuongeza hamu ya sukari.
4. Inatunza afya viungo vya uzazi.
Kina dada, mnafahamu mnaweza kupunguza matatizo ya mabukizi ya fangasi kwa kulala uchi/watupu? Unaweza kupunguza kuzaliana kwa fangasi na uke wako utakushukuru kwa hilo. Vilevile wanaume wanaweza kufaidika kulala uchi/watupu kwa kuwa korodani zinakuwa katika jotoridi la kutosha na uzazi unaongezeka.
5. Mzunguko wa damu unakuwa bora
Hakuna kitu kibaya kama lastiki inayozuia mzunguko wa damu. Ondoa nguo zenye lastiki na utajipata uko na furaha kwa mtiririko wa damu mzuri ndani mwili wako, vile vile inaelezwa kuwa ukiwa hauna nguo inasiaia kutunza ngozi yako kwani inaweza kupumua vizuri.
6. Kutokuwa mvivu
Faida nyingine ni kwamba mara baada ya kuamka unakuwa na ulazima wa kuvaa nguo kwa ajili ya siku hiyo mpya na sio kuamka na nguo zako za kulalia na kutoka nazo nje.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment