Mpambano huo ambao umefanyika nchini Marekani na karibu dunia nzima kufuatilia, uliibua kelele za shangwe pale Mayweather alipomtandika ngumi nzito McGregor iliyomfanya...
arudi nyuma kwenye ulingo, na kumshindilia zingine mbili za kichwa, bila McGregor kurudishia.
Baada ya mpambano Mayweather alisema McGregor ni mshindani mgumu lakini walifanikiwa kuwapa mashabiki walichokuwa wakihitaji.
“Ni mshindani mwenye nguvu na yuko vizuri kuliko nilivyodhani, tumewapa mashabiki walichotaka, lakini nilikuwa mtu bora zaidi, mpango wetu ulikuwa ni kuchukua muda zaidi, acha apige ngumu zake nzito na kumtoa mwisho wake”, alisema Mayweather.
Pamoja na hayo Mayweather ameshtua mashabiki wake huenda asipambane tena ulingoni kwa kusema kuwa pambano hilo ni la mwisho kwake kwa usiku huo.
Mpambano huu unamfanya Mayweather kuweka rekodi ya kuwa 'undefeatable' kwenye pambano aliloshiriki, kwani mpaka sasa atakuwa na jumla ya mapambo 50 aliyopigana na kushinda yote, na kwa kutoa 'knock out' litakuwa pambano la 27.
0 comments:
Post a Comment