Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), limeomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu nchini
kutokana na makosa ya kiuandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa
Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017 kwa klabu ya Simba.
Makosa yaliyoonekana katika ngao hiyo ya jamii ni kukosewa kuandikwa kwa neno “SHIELD” ambapo... liliandikwa “SHEILD” na hivyo kupoteza maana yake ya msingi.
Katika taarifa ya TFF iliyotolewa leo
Agosti 24 wamesema kwamba “Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa
miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekana wenye makosa kwenye
Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.”
Kuonyesha kukerwa na uzembe huo
uliofanywa na baadhi ya viongozi wake, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari
amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika.
Mbali na hilo, kiongozi huyo
amewasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha ngao hiyo ili kufanyiwa
marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi. Uongozi wa TFF umesisitiza kuwa hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.
0 comments:
Post a Comment