Monday, August 21, 2017
NIKKI WA II: TUNAHITAJI MAENDELEO LAKINI UTU LAZIMA UZINGATIWE
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Nikki wa Pili ameguswa na bomoabomoa inayoendelea jijini Dar es salaam kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro kwa kusema tunahitaji maendeleo lakini utu lazima uzingatiwe kwani wanaobomolewa ni watu masikini na maendeleo ni kwa ajili yao.
Nikki wa Pili amesema watu wengi wanaoishi maeneo yaliyokumbwa na bomoabomoa ni watu masikini na wamehangaika kujenga nyumba hizo ambazo...
zinabomolewa kupisha upanuzi wa barabara je, hayo maendeleo yanayofanywa ni kwa ajili ya nani?
“Unaposikia bomoa mara nyingi huwa makazi yà watu wa chini wajuu wakiguswa ni wachache…….basi hayo maeneo yataendelezwa na kuwa ya wakazi wa hali ya juu au maghorofa ya kumilikiwa na wageni au vyovoyote vile……..lakini wale waliokuwa pale mwanzoni hawataweza kuishi pale….watakuwa pembezoni huko au watabaki bila makazi kabisa…je ni maendeleo kwa ajili ya nani? Je maendeleo ni kufukuza tabaka flani la wengi pembezoni kwakuwa hawana kitu”.
Amehoji Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Instagam huku akisisitiza kuwa maendeleo yoyote lazima yawalenge watu hao masikini na sio kuwafukuza.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment