skip to main |
skip to sidebar
VANESSA MDEE ATUA KWENYE IMAYA YA CASSPER NYOVEST
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Vanessa Mdee amezidi kuonyesha uwezo
wake kwa upande wa ‘video queen’ mara baada ya kuonekana katika video
ya rapper Cassper Nyovest kutoka nchini Afrika Kusini.
Juzi,
October 30, 2017 Cassper Nyovest aliachia ngoma yake mpya hiyo ‘Baby
Girl’ ambayo Vanessa...
ndio kachukua nafasi hiyo ‘video queen’.
Hii si mara kwanza kwa Vanessa kufanya hivyo, utakumbuka January 2015
alitokea kwenye video ya Jux katika ngoma ‘Sisikii’, baada ya hapo
waliweza kutoka ngoma ya pamoja inayokwenda kwa jina la Juu.
Hata
hivyo kuna uwezekana mkubwa Cassper Nyovest akapita katika nyayo za Jux
kwa kuja kuachia ngoma na Vanessa. Akizungumza na Dj Show ya Radio One
Vanessa amesema kuna muendelezo wa kazi kati yake na rapper huyo.
“Ni project endelevu tumeanza kwanza na video yake ya ‘Baby Girl’
ambayo nimecheza, so next msubirie kidogo itakuja very soon” amesema
Vanessa.
0 comments:
Post a Comment