Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim
Jong-un amesema kuwa na kibonyezo cha silaha za nyuklia kwenye meza yake
wakati wote na hivyo Marekani isithubutu kuanza vita.
mazungumzo.
Korea Kaskazini pia itatuma kikosi katika mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini, Kim alisema.
Wakati aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu vitisho vya Kim, Rais wa Marekani alisema, "tutaona, tutaona".
Alikuwa akizungumza kando mwa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya katika eneo lake ya kifahari la Mar-a-Lago huko Florida.
- Kim Jong-un aahidi kurusha makombora zaidi Pacific
- Trump: Ningependa kukutana na Kim Jong-un
- Nani alimrukia Kim Jong-un?
- Kim Jong-un: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani
Taifa hilo lililotemgwa lilifanya majaribio 6 ya nyuklia ya chini ya ardhi na kuonyesha kuongeza uwo wake wa makombora Mwezi Novemba ilifanyia majaribio kombora lake la Hwasong-15 ambalo lilipaa umbali wa kilomita 4,475 mara kumi zaidi kuliko kituo cha safari za anga za juu.
0 comments:
Post a Comment