Pages

Subscribe:

Wednesday, January 17, 2018

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya 18) - 18

Related image
Sehemu ya:18
Mark alijibu"hata dada yangu nimemficha suala hili kwani niliamini Suzy ni rafiki yake tangu utoto hivyo nilijua atamueleza suala hili", mama Careen alifurahi sana kumuombea mume wake huyo asiye rasmj baraka zote kwa Mungu nakuanzia siku hiyo mama Careen alitunza mali zote za Mark. 


Mama Prisca alifika nyumbani na mume wake, walirudi hospitali alipompa daktari ile barua, daktari alisikitika sana lakini hakua na namna ilibidi mtoto apewe...
dawa na kuwasisitiza kumpa ziwa kwa wakati na kurudi hospitali mara kwa mara ili kujua maendeleo ya mtoto, mama Prisca hawakua na namna zaidi ya kukubaliana na kile kilichopo, mtoto alianza kunywa dawa. 

Inasikitisha sana kwani mtoto alikua bado mdogo sana lakini hawakua na jinsi. Maisha yaliendelea kama kawaida miaka nayo ilikua inakimbia sana kwani miaka 6 sasa ilikua imepita na maisha ya Prisca yaliendelea kua yakunywa dawa mpaka umri huo. Alikua na afya dhoofu sana. Na wakati huo mzee Moto alikua mzee sana miaka hiyo. 

Mark aliendelea na maisha yake ya taabu na Suzy kwani tayari mambo yake yalikua hayaendi kama zamani, na kipindi hicho tayari mke wake alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Samson. 

Mark alijitahidi sana katika kazi lakini hali haikua nzuri japo alimfungulia mama Careen biashara na ndiye aliyekua akimtia nguvu kuna wakati mama Careen alishauri waende kanisani lakini Mark alisema "usijali mama yangu unajua mambo mda mwingine yakua si sawa lakini kuna kipindi hua yananyooka vizuri sana kwahiyo naimani yatakua sawa, ila nimegundua mama Samson ana mwanaume mwingine kwani siku hizi nyumbani hapakaliki nikimuuliza anakua mkali niombee tu mama", 

Mama Careen alisikitika akasema "Mark rudi nyumbani kakae uongee nae kwani siku hizi maradhi mengi tusije uana bure", mark alijibu"nalifahamu hilo mama ila mimi nataka niachane nae kabisa nikuoe wewe tena kwa ndoa, mama Careen alijibu"mimi sina la kusema yote mipango ya MUNGU itakavyo kua ndivyo kwahiyo tuzidi kuomba na tusilazimishe mambo mume wangu, mimi nimeridhika tu kuishi hivi na wewe liwalo na liwe". Mark alimpenda sana mama Careen kwake alikua ndiyo kila kitu, basi alianza safari ya kurudi kwake ili akazungumze na mama Samson, 

Usikose 19

0 comments:

Post a Comment