Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema kutokana na kuingia kwenye uhusiano na wanaume tofauti akiwemo mfanyabiashara maarufu, Dallas ambao ameshindwa kufanya nao... maisha, anahitaji mtu ambaye kweli atajiridhisha kuwa anafaa kuwa mume na si vinginevyo.
Alipoulizwa kuhusu Daktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asilia, Dk. Fadhili Emily ambaye alitajwa kuhusika kuvunja uchumba wake na Mkongo, Wolper alisema muda bado wa kumzungumzia daktari huyo.
“Huyu nimefahamiana naye muda si mrefu hivyo hata kama ni yeye nitahitaji muda kidogo kujiridhisha nione kama anafaa,” alisema Wolper.
Chanzo: GPL
0 comments:
Post a Comment