Pages

Subscribe:

Monday, August 7, 2017

MAAJABU YA NGORONGORO SIMBA KUMNYONYESHA MTOTO WA CHUI


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imesema picha ambazo zinamuonyesha simba jike akimnyonyesha mtoto wa chui ni moja kati ya matukio ya ajabu ambayo yanatokea katika hifadhi hiyo. Picha hizo ambazo zilisambaa katika mitandao ya kijamii na kuibua gumzo huku wengi wakishangazwa na kitendo hicho kisicho cha kawaida katika ulimwengu huu.

Kwa mujibu wa BBC wanyama hao walionekana na...
Joop Van Der Linde mgeni katika katika eneo la Ndutu safari Lodge nchini Tanzania katika eneo la uhifadhi la wanyama pori la Ngorongoro.

Akiongea na Bongo5, Afisa Hifadhi wa Ngorongoro, Peter Makutian, alisema tukio hilo huwenda ni kweli limetokea katika hifadhi hiyo kutokana na matukio mengi ya ajabu ambayo yamekuwa yakitokea katika hifadhi hiyo.

“Ngorongoro kuna mambo mengi sana ambayo hata ukisimuliwa nje hauwezi kuamini, kama hilo tukio la Simba kumnyonyesha mtoto wa chui ni matukio ambayo ni magumu kutokea katika maisha ya wanyama hao lakini likitokea linakuwa ni tukio la kishistoria,” alisema Peter.

Aliongeza, “Kama nilivyosema hatuna taarifa rasmi lakini wengi ambao wameona hiyo picha wanasema ni Ngorongoro, ile picha siyo ya kutengenezwa na kama unavyojua Ngorongoro pia ni makazi ya watu kwahiyo kuwenda kati ya watu ambao wanaishi pale walishuhudia tukio hilo na kuamua kulipiga picha au wagon ambao wanakuja kila siku,  lakini kwetu sisi hilo ni tukio la ajabu sana kwa sababu wanyama hawa hawapiki chungu kimoja, kila mmoja anamaisha yake na tabia zake ingawa ni wanyama ambao wapo kwenye kundi moja la wanyama wala nyama,”

“Lakini yapo matukio ambayo yatokea kwa nadra na katika mazingira ya kustajabisha kama tukio hilo lakini ndani ya Ngorongoro kuna matukio mengi ya namna hiyo. Kwa mfano katika maisha ya Simba na Chui hawa ni wanyamba ambao kila mmoja anaweza akamuua mwenzake lakini hamli, lakini ndani ya Ngorongoro Simba walimuua chui na kumla kitu ambacho si chakawaida kutokea katika maisha ya hawa wanyama,” alifafanua zaidi Peter.

Kwa upande wa Balozi wa Ngorongoro, Mrisho Mpoto amesema yeye kama balozi katika kipindi hiki cha Nane Nane amewataka wakazi wa Arusha kuchangamkia ofa iliyotolewa na Ngorongoro ya kutembelea hifadhi hiyo kwa tsh 50,000.

Mrisho Mpoto akifafanua jambo pamoja na wafanyakazi wa Ngorongoro
“Huu ni wakati wa kila mtu kwenda Ngorongoro, hii ni fursa nzuri kwa wakazi wa Arusha kwa sababu kama mlivyosikia ni elfu 50000 tu. Hiyo ni kwaajili ya chakula, usafiri pamoja na mtu ambaye atakuongeka katika kila sehemu. Kwahiyo kweye hili mimi naona hii ni fursa nzuri kutoka Ngorongoro ambapo kuanzia kesho tarehe 6 tripu ya kwanza na kuendelea tarehe 7 na 8,”

0 comments:

Post a Comment