Msanii wa maigizo aliyefanya vizuri na filamu ya 'Mapenzi ya Mungu',
Elizabeth Michael ' Lulu' amefunguka na kusema wasanii wa maigizo bongo
wanafeli kutokana na kutojielewa ni kitu gani ambacho wanakitaka kwenye
sanaa, badala yake wanafuata mikumbo.
Lulu
amefunguka hayo hivi karibuni akizungumza na wanahabari na kusema kuwa
wasanii wengi wa Tanzania hawapendi...
kujishughulisha kutafuta kitu kizuri
kwa kuwa wengi wao walifuata mkumbo kwenye kuigiza na wengine
walichukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu ili maisha yaendelee
au sehemu ya kupotezea muda.
"Ukweli upo kwenye uigizaji
kuna watu tunachukulia hii ni kazi, wapo wanaofanya kama sehemu ya
kipaji chake lakini pia wapo ambao wanachukulia kama sehemu ya kujipatia
umaarufu au ku-refresh kwani wanakua na kazi zao zingine, na hao ndio
wanaosababisha tuonekane waigizaji wa muvi tumefeli".
Pamoja na hayo Lulu ameongeza, "Unajua
pia kufuata mkumbo ni kitu kilichoturudisha nyuma. Watu wengi walikuwa
wanaangalia mafanikio ya mtu mmoja na wote tukawa tunapita njia zilezile
ili tufanikiwe badala ya kutafuta za kwetu ndiyo kama mnavyoona sasa
hivi tunalalamika lakini mashabiki zetu wanatusapoti hivyo japo
tunawakwaza".
Akizungumzia kuhusu wasanii wa Nigeria
walivyoweza kufanikiwa katika filamu zao, Lulu amesema ni pamoja na
upendo na ushirikiano wanaoonyeshana katika kazi zao na kuongeza kwamba
pamoja na kufanya kazi zenye ubora wa kimataifa watu hao hawajasahau
utamaduni wao.
Kuhusu sababu za wasanii wa filamu
kutokaa 'Location' kwa muda mfupi kutengeneza filamu zao kwa usahii
muingizaji Lulu amefunguka na kusema changamoto kubwa huwa ni bajeti kwa
wasanii hao.
"Bajeti zetu ni tatizo. Bado
hatujawa na uwezo wa kuweka bajeti kubwa kwenye filamu ndiyo maana
tunaomba tuwezeshwe ili tufanye kazi zenye ubora. Kuna vitu ambavyo sisi
pia tunavifanya kwa mapungufu kwa sababu hatuna uwezo wa kumpatia pesa
mtu sahihi wa kufanya kazi husika ndiyo maana unakuta tunafanya kazi kwa
uwezo wetu tu.
0 comments:
Post a Comment