Msanii Jah Prayzah wa Zimbabwe amejikuta katika dhahama kubwa baada ya
wananchi kuanza kumshushia kipigo na mawe, baada ya kwenda kuhudhuria
msiba wa aliyekuwa mlinzi (Body guard) wake.
na meneja wake, ndipo wananchi waliokuwa kwenye shughuli ya mazishi kuanza kumvamia kwa kipigo huku wengine wakimrushia mawe wakimlaumu kwa kifo cha marehemu.
Meneja wa msanii huyo Keen Mushapaidze amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba..”Tulikwenda kutoa heshima zetu za mwisho na ndipo waombolezaji walipotushukia, hatukujua kuwa baadhi ya waombelezaji walikuwa na hasira, hatujui kama ni sababu hatukuchagia chochote kwenye msiba au mahusiano yetu na Crispen”.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo habari zimeeleza kuwa waombolezaji hao walilazimika kusitisha kwanza shughuli za mazishi na kuweka sanduku chini.
Mwanamuziki huyo baada ya kuona hali inazidi alikimbilia mahali ambako gari ale lilipaki na kuingia, na kisha kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.
0 comments:
Post a Comment