Tunaelekea msimu wa sikukuu za Xmass na mwaka mpya na dunia nzima iko
na mihangaiko kuelekea siku hizi kubwa za mwaka, lakini hali kwa kiungo
wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ivory Coast Emmanuel Eboue ni
tofauti kabisa.
Taarifa zinasema Eboue anataka kufanga jaribio la kujiua kutokana na
hali mbaya inayomkabili katika maisha yake, ripoti zinasema kiungo huyo
ameyumba sana kiuchumi kiasi cha kuona...
uhai hauna thamani tena kwake.
Eboue alikuwa akipokea kiasi kikubwa katika klabu ya Arsenal huku
akipokea zaidi ya £1.5m wakati akiichezea klabu ya Galatasaray lakini
inasemekana kwamba talaka na mkewe huenda ikakomba kila kitu
alichonacho.
Talaka kati ya Eboue na mkewe aliyetambulika kwa jina la Aurellie
imemfanya Eboue kuwa na msongo wa mawazo mkubwa unaochangiwa na
kuzuiliwa kuwatembelea watoto wake watatu Mathis, Clara na Maeva katika
msimu huu wa Xmass.
Inafahamika kwamba Eboue alimpa mamlaka na haki ya kumiliki mali zote
walizokuwa nazo na kitendo ya kutalakiana kinamaanisha Eboue atapoteza
kila kitu alichomuandikishia mwanamke huyo baada ya kushindwa kesi ya
talaka mahakamani.
Achana na majanga hayo ya Eboue lakini mchezaji huyo alitoka kufiwa
na babu yake nchini Ivory Coast aliyefariki kwa kansa huku kaka yake
aliyefahamika kwa jina la N’Dri Serge naye alifariki kwa ajali ya
pikipiki.
Matatizo ya Eboue ya umiliki wa baadhi ya vitu ikiwemo nyumba yake ya
kisasa iliyoko London na hana pesa ya kuwalipa watetezi wa kisheria
hali ambayo inakaribia kupelekea baadhi ya nyumba na mali alizobakiwa
nazo kuuzwa.
“Naogopa hata watu kufahamu kwamba niko ndani, sina amani nikiwa
ndani maana nawaza muda wowote polisi wanaweza kuja kuniondoa, siwashi
hata taa maana sitaki watu nje wajue kwamba nipo” alisema Eboue.
Mbaya zaidi Eboue amesema amekuwa na mawazo ya kujiua kwa sasa
kutokana na hali ilivyobadilika katika maisha yake na amekuwa akimuomba
mungu sana amuondolee mawazo hayo mabaya kichwani mwake.
Akielezea kwa majonzi makubwa sana Eboue anakumbuka namna alivyotoka
katika mazingira magumu hadi kupata pesa na kisha kununua nyumba lakini
sasa hana amani katika nyumba yake mwenyewe.
Eboue analala katika nyumba ya rafiki yake ambapo inasemekana analala
chini huku hana hata pesa ya kupelekea nguo dry cleaner hali
inayompelekea kutumia mikono yake kufua nguo.
Eboue anasikitisha sana na amesema anatamani klabu yake ya zamani ya
Arsenal imsaidie katika kipindi hiki kigumu lakini atajisikia vibaya
kama akionana na wachezaji wenzake wa zamani akiwemo Thiery Henry.
Dunia imeshtushwa sana na habari za kiungo wa zamani wa
Arsenal na timu ya taifa ya Ivory Coast, wengi wamekuwa wakihoji
inakuwaje nyota mkubwa kama huyo ambaye amewahi kuwa tajiri mkubwa
kuanguka kiuchumi.
Inafahamika kwamba Emmanuel Eboue wakati akicheza soka lazima alikuwa
na marafiki wakubwa ambao walikuwa na uwezo mkubwa sana kifedha ikiwemo
wachezaji na hata kocha wa Arsenal Arsene Wenger, kwa nini hawamsaidii?
“Wakati wa matatizo haya yakiendelea nilipoteza simu yangu ambayo
kulikuwa na namba nyingi, Wenger tulikuwa tukiongea lakini tangu
nipoteze simu sijawahi kuwasiliana naye pamoja na marafiki zangu”
anasema Eboue.
Eboue
anasisitiza kwamba kwa sasa anapokea msaada kutoka kwa mtu yeyote
lakini kama vilabu ambavyo alikuwa akivitumikia awali Galatasaray au
Arsenal wataamua kumsaidia baasi atafurahi sana.
Eboue anasema ana ndoto za kurudi Arsenal kuwasaidia wachezaji wadogo
na kwa sasa hataki kazi kubwa sana kwani hata kazi ndogo tu
itakayompatia kipato kidogo itakuwa muhimu sana kwake katika kipindi
hiki.
Eboue anasema anataka kuendelea kucheza soka lakini pia akasema
ataona aibu kama akipewa kazi ya kuwafundisha vijana wa Arsenal halafu
akakutana na wachezaji ambao zamani alicheza nao ataona aibu.
Mashabiki mtandaoni wameibuka na wakimpa pole kwa lililompata na huku
wengine wakienda mbali kwa kuiomba klabu ya Arsenal kutoa msaada kwa
kiungo wao huyo wa zamani.
Pamoja na yote na pia ni somo kwa vijana wa Kiafrika lakini Emmanuel
Eboue haachi kumshukuru Mungu na amesema yote yanayoendelea katika
maisha yake ni mpango wa mungu na hatamani yamtokee mtu mwingine.
Monday, December 25, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment