Faida za limau au ndimu zinajumuisha matumizi kama tiba kwa ajili ya
vidonda vya kooni, matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya
meno, homa, kuvuja damu ndani ya mwili, baridi yabisi, kutibu
malengelenge, uzito kupita kiasi, matatizo katika mfumo wa upumuwaji,
kipindupindu na shinikizo la juu la damu. Pia ni dawa nzuri kwa ajili ya
nywele na ngozi.
Tangu karne nyingi limau linajulikana kama dawa, husaidia pia kuongeza
kinga ya mwili, kusafisha tumbo na hujulikana pia kwa kazi yake nzuri ya
kusafisha... damu.
Juisi ya limau ina faida kadhaa nyingi kama vile kuondoa mchanga
katika figo, kupunguza kukamaa kwa mishipa (strokes) na kupunguza joto
la mwili. Kama kinywaji ambacho huondoa uchovu mwilini, juisi
ya limau itakusaidia kubaki mtulivu na mpole.
Faida nyingi za limau zinatokana na virutubishi vyake vingi mhimu kwa
mwili kama vile vitamini C, vitamini B6, vitamini A, vitamini E, folate,
niacin thiamin, riboflavin, pantothenic acid, shaba, kalsiamu, chuma,
magnesium, potassium, zinki, phosphorus na protini.
Limau ni matunda ambayo yana kitu mhimu sana katika kuondoa sumu
mwilini kiitwacho kwa kitaalamu kama “flavonoids” ambacho chenyewe ni
mhimu sana katika kupigana na kansa mbalimbali mwilini.
Limau husaidia pia kuzuia matatizo ya kisukari, kufunga choo, shinikizo
la juu la damu, homa, husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya
kazi vizuri na matatizo mengine mengi yakiwemo kuimarisha ngozi ya
mwili, nywele na meno.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya mfumo wa mkojo cha Marekani (American Urological Association) unaonyesha kuwa juisi ya limau au ‘lemonade’ inaweza kuondoa au kuzuia kujitokeza kwa mawe kwenye figo.
Watu hutumia limau kutengeneza juisi ya limau maarufu kama “lemonade”
kwa kuchanganya pamoja maji maji ya limau, maji na asali au hata sukari
ya kawaida. Watu wengi pia hutumia limau katika kusafisha au kuosha
vyombo sababu ya uwezo wa kuondoa madoa na uchafu mwingine kirahisi
zaidi.
Marashi au harufu ya limau hufukuza mbu, wakati huo huo kuinywa juisi
ya limau iliyoongezwa mafuta ya zeituni husaidia kuondoa mchanga katika
kibofu cha mkojo. Limau inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi na
hutumika kwa namna nyingi tofauti.
Zifuatazo ni faida mbalimbali za limau mwilini:
1. Kufunga choo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula
Juisi ya limau husaidia kutibu matatizo yahusianayo na tumbo kushindwa
kumeng’enya chakula na kufunga choo. Ongeza matone machache
ya limau kwenye chakula chako (kuwa makini sababu limau huwa haipatani
na maziwa), na itakusaidia katika kumeng’enya chakula.
Limau hufanya kazi kama wakala msafisha damu na mwili kwa ujumla. Na hii
ni nzuri kama unapata juisi yako ya limau baada ya chakula cha mchana
au cha usiku. Juisi ya limau inatengenezwa kwa
kuchanganya maji ya limau, maji kidogo, chumvi ya mawe kidogo
na asali au hata sukari. Weka na barafu kidogo pembeni.
Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari
(fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii
kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.
2. Hutibu homa
Juisi ya limau inaweza kumtibu mtu anayesumbuliwa na homa, mafua au
baridi. Limau husaidia kutibu homa kutokana na sifa yake ya kuongeza
kiasi cha jasho mwilini.
3. Huongeza afya ya meno
Juisi ya limau mara nyingi imetumika katika kulinda afya ya meno. Kama
juisi fresh ya limau itanyunyizwa juu ya jino linalouma inaweza kusaidia
kuondoa maumivu. Kusugua (masaji) juisi ya limau juu ya fizi za meno
kunaweza kusaidia watu wenye matatizo ya kutokwa damu kwenye fizi huku
ikiondoa harufu mbaya katika fizi na mdomo kwa ujumla.
Unaweza kupata faida hizi kama utakuwa unapiga mswaki ukitumia dawa yenye limau ndani yake (lemon tooth paste).
4. Hutunza nywele
Juisi ya limau imejidhihirisha yenyewe kuwa dawa nzuri kwa upande wa
matatizo mbalimbali ya nywele. Juisi ya limau ikipakwa kwenye ngozi ya
kichwa inaweza kutibu matatizo kama ya mba, kupotea au kukatika kwa
nywele, na matatizo mengine yahusuyo nywele na ngozi ya kichwa.
Kama utakuwa ukisafisha nywele zako kwa kutumia juisi
au maji ya limau moja kwa moja basi utazifanya nywele zako zipate
mng’aro wake wa asili bila gharama yoyote ya ziada.
5. Hulinda ngozi
Kwakuwa Juisi ya limau ni dawa ya asili dhidi ya bakteria, inaweza pia
kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi. Juisi ya limau inaweza kutumika
kupunguza maumivu kwenye ngozi sababu ya kuungua na jua, pia husaidia
kupunguza maumivu kutokana na kung’atwa na nyuki. Juisi ya limau au
majimaji ya limau yanaweza kutumika kupakaa juu ya ngozi na kutibu
chunusi na ukurutu.
Limau pia hutumika kama dawa ya kukufanya usionekane mzee kwakuwa yenyewe huondoa mikunjo na madoadoa ya ngozi.
Kunywa maji ya limau yaliyochanganywa na asali kunasaidia ngozi kuwa
na afya zaidi na hata ukipekuwa huko sokoni utazipata baadhi ya sabuni
ambazo zimetengenezwa kutokana na limau.
6. Hutibu majeraha ya moto
Upakaji
wa maji ya limau (juisi) kwenye eneo la ngozi lililoungua huweza
kusaidia makovu kupotea na hii husaidia pia kwa mtu aliyepatwa na
malengelenge au vipele vyenye maji maji yanayouma ndani. Na kwa
sababu limau ni wakala wa kupooza au wakala mtulizaji (cooling agent), huweza kupunguza maumivu au kuhisi kuungua kwenye ngozi hasa wakati unakuwa na majeraha yanayounguza ngozi.
7. Huzuia kuvujika kwa damu
Limau inayo sifa ya kudhibiti bakteria mwilini (antiseptic properties)
na kugandisha damu, sifa hizi au kazi hizi mbili za limau husaidia
kusimamisha kuvuja kwa damu ndani ya mwili. Unaweza
kutumia maji ya limau ukiweka kwenye kipande cha pamba na kuiweke puani
kuzuia pua kuvuja damu.
8. Hupunguza Uzito
Ikiwa utakunywa juisi ya limau iliyochanganywa na asali na maji ya
uvuguuvugu, hasa asubuhi tu unapoamka inaweza kusaidia kupunguza uzito.
9. Hutibu matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
Juisi ya limau husaidia katika kutuliza matatizo katika mfumo wa
upumuwaji kama vile pumu. Kwakuwa limau ina kiasi kingi cha vitamini C,
husaidia kutibu na kutuliza matatizo ya muda mrefu kwenye mfumo wa
upumuwaji.
10. Kipindupindu
Magonjwa kama kipindupindu na malaria yanaweza kutibika kwa kutumia
juisi ya limau tu kwa sababu limau hufanya kazi ya kusafisha damu na
mwili kwa ujumla.
11. Hutuliza maumivu ya miguu
Limau huwa na harufu ya kuvutia (aromatic) na pia inayo sifa ya
kudhibiti bakteria na hutumika kutuliza maumivu au miguu kuwaka moto.
Ongeza juisi (maji ya limau) kwenye dishi lenye maji ya moto kidogo na
utumbukize miguu kwa dakika kadhaa kwa kuondoa haraka maumivu ya miguu
na utajisikia umepata tulizo fulani (relaxed).
12. Baridi Yabisi
Limau au ndimu pia ni kikojoshi, yaani ni kitu kinachosisimua
uzalishwaji wa mkojo na kwa sababu hiyo inaweza kutibu baridi yabisi na
maumivu ya kwenye mishipa. Husaidia kutoa nje bakteria wabaya na sumu
mbalimbali mwilini.
13. Hutibu malengelenge (Corns)
Juisi ya limau inaweza kusaidia kukausha malengelenge au vipele ambavyo
huwa na majimaji ambavyo hujitokeza mara nyingi chini ya unyayo au
katikati ya vidole vya mikono. Kunywa juisi ya limau na maji ndani yake
husaidia wagonjwa kupunguza mawe kwenye nyongo.
14. Hutibu maambukizi ya kwenye koo
Limau ni tunda bora kabisa ambalo hupigana dhidi ya matatizo
yanayohusiana na maambukizi kooni sababu ya sifa yake kubwa ya kudhibiti
bakteria mwilini.
15. Hutibu shinikizo la juu la damu
Kunywa juisi ya limau kuna msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya moyo
kwa sababu limau lina kiasi cha kutosha cha potasiamu. Limau hudhibiti
shinikizo la juu la damu, kizunguzungu, na uchovu sugu kwa sababu
yenyewe limau hutoa hisia za utulivu kwa mwili na roho pia. Mara
nyingi limau imetumika kwa watu wenye mfadhaiko wa akili na majonzi.
0 comments:
Post a Comment