Msanii wa muziki wa bongo fleva Mr. Paul ambaye kwa sasa anaishi nchini
Australia, amekiri kutokea kwa tukio ambalo lilimdhalilisha sana siku
za nyuma mpaka kuandikwa kwenye magazeti, na kusema ni kitu ambacho
hatokisahau na ilikuwa aibu kubwa kwake.
AKizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, Mr. Paul amesema tukio hilo la kuandikwa kwenye magazeti kuwa amekuwa chapombe mpaka kufikia hatua ya...
kulala baa, lilitokana na kunywa pombe baada ya kutoka kumsindikiza mkewe alivyoondoka nchini.
"Nilikuwa nimetoka kumsindikiza mke wangu uwanja wa ndege, nikarudi nikapaki gari lioshwe, nilikuwa sijala chakula nikakutana na marafiki, tukaanza moja mbili tatu bila kula, nikasema ngoja nijiegeze kidogo kwenye viti vya baa, Kilichotokea sielewi, kwa sababu nimeamka nipo home, naona headlines kwenye magazeti jamaa kalewa analala baa sikatai ilitokea, nilikuwa ni aibu, samahani kwa mashabiki wangu, ilikuwa tukio la maramoja tu lakini sio kama cha pombe", amesema Mr. Paul.
Pamoja na hayo Mr. Paul ameomba radhi mashabiki wake kwa tukio hilo, na kusema kwamba lilitokana na stress za kummisi mkewe ambaye alisafiri.

0 comments:
Post a Comment