Pages

Subscribe:

Saturday, December 23, 2017

UNAFAMU KUWA MWILI WA NZI UNA AINA 600 ZA BAKTERIA

Inafahamika kuwa nzi ni wachafu na hueneza magonjwa mbalimbali, lakini je umeshawahi kufahamu kuwa nzi hubeba viini vingi vinavyosababisha magonjwa kuliko inavyodhaniwa?

Utafiti mpya uliofanyika siku za hivi karibuni na Chuo Kikuu cha Pennsylvania Marekani umebaini kuwa nzi huwa na bakteria zaidi ya aina 600 kwenye miili yao kwa wakati mmoja. Hii imegundulika baada ya...
wanasayansi kufanya vipimo vya DNA kwa nzi.

Nzi husababisha maradhi mengi kwa binadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya tumbo, sumu kwenye damu na nimonia pia hueneza bakteria kutoka eneo moja hadi jingine kwa kutumia miguu yao na madawa.

0 comments:

Post a Comment