Mtendaji
mkuu wa kampuni ya Apple, Tim Cook, amewaomba radhi wateja wake
kuhusiana na kwamba simu za kampuni hiyo hupungua nguvu za utendaji wake
kutokana na betri zinazoisha muda wake haraka.
Cook ameahidi kwamba, siku zijazo,
Apple “itatoa kipaumbele zaidi kuhusiana na nguvu ya betri za simu aina
ya iPhone” na kuwaacha watumiaji wake waone iwapo muda mrefu wa betri
hizo utaathiri...
utendaji wa simu zao. Apple inatoa punguzo katika
manunuzi ya betri mpya kwa yeyote mwenye iPhone 6 au nyingine, ilisema
kampuni katika taarifa yake.
Betri mpya itagharimu Dola 29 (Tsh.
58,000) badala ya Dola 79 (Tshs 176,000) kuanzia Januari mwaka 2018.
Punguzo hilo linatia maanani pia mahitaji ya maduka ya watengenezaji wa
simu. Wakati ujumbe huo wa Cook ulikuwa unawataka radhi wateja, bado
alikana kwamba Apple hupunguza kasi ya utendaji wa simu hizo ili
kuwalaziisha watu kununua simu mpya.
“Kitu cha kwanza na muhimu zaidi ni
kwamba kamwe hatujafanya na hatutafanya chochote cha kupunguza makusudi
muda wa utendaji kazi wa bidhaa za Apple, au kumlazimisha mteja anunue
bidhaa nyingine,” alisema. Kampuni hiyo huko nyuma iliwahi kusema kwamba
iwapo isingepunguza utendaji kazi wa simu hizo, betri za zamani
zilikuwa zinakabiliwa na tishio la kuzima ghafla.
Kwa mujibu wa wataalam, maelezo hayo
yalikuwa ya kiufundi. Tamko hilo la Apple la wiki iliyopita kwamba
hupunguza utendaji kazi wa simu hizo, liliibua shutuma nyingi na watu
kufungua kesi. Kampuni moja ya Ufaransa inayopigania haki za wateja,
ilifungua kesi wiki hii (Desemba 27) kuishitaki Apple kwa kupunguza
nguzu za simu zake za zamani ili kupata fursa ya kuuza mpya.
Nchini Ufaransa, ni haramu kupunguza
ubora wa bidhaa za zamani ili kupromoti mauzo ya bidhaa mpya. Kesi hiyo
iliyofunguliwa na kundi la Halte à l’Obsolescence Programmee, ina
uwezekano wa mshitakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.
Sunday, December 31, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment