Pages

Subscribe:

Tuesday, January 2, 2018

ALIKIBA: NINAPO TAFUTA MWANAMKE HUWA NAANGALIA RANGI NA UZURI WA SURA

Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake 'Maumivu Per Day' amefunguka na kutaja sifa mbalimbali za mwanamke ambaye anamchanganya, kumpenda na kusema moja ya sifa yake ni weupe. 

Alikiba ameonekana akizungumzia hayo akiwa na mtangazaji wa kipindi cha NIRVANA, Deogratius Kithama katika promo ya show hiyo itakayoruka leo usiku na kusema kuwa uzuri wa sura kwa mwanamke, weupe pamoja na...
kujaaliwa ni kati ya vigezo ambavyo yeye huangalia pindi anapomtafuta mtu wa kuwa naye kwenye mahusiano.

Mbali na hilo Alikiba atazungumzia juu ya maisha na makuzi yake kabla ya kuwa maarufu lakini pia atagusia maisha yake ya mapenzi na kumuongelea mtu ambaye yupo naye sasa kwenye mahusiano bila kusahau style za mavazi anayopendelea.

Usikose kutazama uzinduzi wa msimu mpya wa NIRVANA kwa mahojiano haya maalum na Alikiba leo kuanzia saa tatu usiku kwenye ting'a namba moja kwa vijana EATV.

0 comments:

Post a Comment