Pages

Subscribe:

Wednesday, November 4, 2015

ALIKIBA NA CHRISTIAN BELLA KUZINDUA WIMBO WAO IJUMAAHII


Ijumaa ya wiki hii Alikiba na Christian bella watakata kiu ya mashabiki wao kwa kuachia collabo yao inayosubuliwa kwa hamu zaidi.
Kwa upande mwingine, Alikiba na Christian bella wamesema story ya wimbo wao inavutia kiasi kwamba unaweza tengenezea filamu lakini awe na Million 700 mezani kwa sababu...

Bella na Ali Kiba
“Nyimbo tuliyoimba inaweza ikawa hata sound track ya movie kwasababu ni story ambayo inavutia, inapendeza…” Alikiba alifunguka kupitia 255 ya XXL. “Ni idea nzuri ambayo inahitaji hata kufanyiwa movie ikipata nafasi vile vile uwezekano huo wa kufanya upo.

Kiba na Bella wametoa nafasi kwa mtu ambaye atapenda kutengeneza filamu kupitia idea ya wimbo wao lakini awe na Million 700 mezani kwasababu washasajili wazo lao.

“Akija na mtonyo akiweka mtonyo tutafanya tu” alisema Bella. “Kwa haraka haraka labda milioni 700 hivi” aliongezea Kiba.

0 comments:

Post a Comment