Akitoa tamko hilo mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam jana asubuhi, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya gesi yote iliyogunduliwa nchini ni... trioni 57.23.
"TPDC imerekebisha muundo wake tunataka iwe inajishughulisha na utafutaji wa gesi ya mafuta hivyo kufuatana na sheria ya petroli ya mwaka jana kazi zote zitasimamiwa na TPDC na haitaendelea kusimamia makampuni mengine badala yake tuameazisha wakala wakusimamia kazi ," alisema Muhongo.
Akitolea ufafanuzi kuhusiana na kugundulika kwa gesi hiyo asilia iliyopo nchi kavu imefikia futi za ujazo tirioni 10.17, na baharini katika kina kirefu cha futi za ujazo ni 47.08.
Waziri Muhongo alisema ufumbuzi huo umefanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL) hivyo wakiendelea na utafiti wataweza kuvuka hata futi 10 kama walivyo dai.
Alisema kuwa takribani futi za ujazo elfu moja zina uwezo wakuzalisha jumla ya megawati za umeme zipatazo 5000 wakati huo bado wanaendelea na utafiti wa gesi katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ambapo kumegundulika kuwa na gesi nyingi .
"Nilazima taifa letu liwe na umeme mwingi, na umeme wa kutosha kwani tukifanya hivyo tunaweza kufikia kwenye bigawati kama nchi za kusini walivyoweza kupata umeme mwingi," alisema Muhongo.
Akijibu maswali kuhusiana na kunufaika kwa wananchi na gesi hiyo alisema tayari wameaza kunufaika kwani kabla ya awamu ya tano ya Rais Dk. Jonh Magufuli, jumla ya megawati 700 hadi 800 ndizo zilikuwa zikitumika katika matumizi ya umeme ambapo katika kipindi cha awamu ya tano jumla megawati 1000 zinaendelea kutumika.
"Ifahamike kuwa faida ya gesi kwa wananchi ni ya siku nyingi kwani viwanda takribani 37 vimekuwa vikitumika kwa matumizi ya gesi kikiwemo kiwanda cha Saruji " alisema.
Awali kabla ya uzinduzi huo Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi (TPDC), Venosa Ngowi alisema wanatarajia kumpatia ripoti ya mapendekezo ya juu ya gharama za uuzaji wa gesi nchini ifikapo Aprili,20 mwaka huu.
Ngowi alisema zoezi linalofanyika ni mazungumzo ya wawekezaji na watalamu wa nchi husika kuweza kufanya uhakiki wa gharama wa bei za gesi nchini.
Alisema moja ya changamoto wanazokutanazo ni kuwepo kwa gharama nyingi zinazo muhusu mwekezaji.
0 comments:
Post a Comment